Monday 22 December 2014

SOMA ATHARI ZA MAGONJWA YA ZINAA NA UYAEPUKE



Miongoni mwa mambo yanayosababisha maambukizi ya magonjwa ya ngono ni pamoja na kujamiiana bila kondomu kwa njia ya ukeni, haja kubwa au mdomoni, kuzaliwa na maambukizi, kuongezewa damu yenye maambukizi, ulevi wa kupindukia unaomfanya mtu asifanye maamuzi sahihi ya kutumia kinga wakati wa kujamiiana, kurithi wajane au mira na desturi za mwanamke mwenye mali kuoa msichana mdogo na kumtafutia mwanaume wa kuzaa naye watoto (nyumba ntobu) na kujamiiana na watu wanaotumia madawa ya kulevya.

Athari za magonjwa ya ngono ni pamoja na kuharibika mimba mara kwa mara, mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi, ugumba, kuziba kwa mirija ya uzazi, madadiliko ya hedhi, kujifungua kabla ya mimba kutimiza muda wake, kansa ya uume, kupungua nguvu za kiume, utasa, kuziba njia ya mkojo, magonjwa ya akili na maambukizi katika kokwa za mbegu za uzazi.

No comments:

Post a Comment

.