Wednesday 24 December 2014

SOMA MADHARA 20 YA POMBE NA UYAEPUKE.

Pombe za aina zote zina kemikali ambazo baadhi ya hizo kemikali huwa ni sumu mwilini,hivyo kuacha athari ya kiafya kwa mtumiaji.Pombe inaweza ikamdhuru mtumiaji kwa kumsababishia madhara yafuatayo:

1.Vidonda vya tumbo.
2.Kansa ya utumbo.
3.Kusinyaa kwa Ini.
4.Kansa ya Ini.
5.Kansa ya umio(oesophagus)
6.Vindonda kwenye mapafu.
7.Utapiamlo hasa wale wanaokunywa huku lishe duni.
8.Matatizo ya ganzi miguuni na mikononi(Peripheral Neuropathy).
9.Kisukari.
10.Figo kushindwa kufanya kazi.(Renal failure)
11.Kansa ya figo
12.Kukosa au upungufu wa hamu ya tendo la ndoa.(Loss of Libido)
13.Upungufu wa nguvu za kiume.
14.Kuongeza kasi kwa baadhi ya magonjwa hata kama unatumia dawa kama vile Kifua Kikuu,Kansa,Kisukari,Shinikizo la damu la kupanda.n.k
15.Kukosa hamu ya kula.(Anorexia)
16.Kutovyonzwa vyema kwa chakula(Malabosorption)
17.Ugonjwa wa kongosho.(Pancreatis).
18.Magonjwa ya moyo.
19.Mwili kutetema(Tremors)
20.Kichaa cha pombe(mtu hawezi kufanya kazi bila ya pombe,au anakuwa kama mgonjwa lakini akipewa pombe tu anakuwa mzima)

No comments:

Post a Comment

.