Kampuni ya Belly Armor imeanza kutengeza nguo za ndani za wanaume ambao zinawalinda
kutokana na athari ya madini ya chuma yanayoweza kupunguza nguvu za
kiume na kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume hali ambayo inaweza
kusababisha mwanaume kukosa kuzalisha.
Mnamo mwaka 2011, shirika la afya duniani lilitaja madini hayo hatari
ikiwemo miale inayotokana na simu za mkononi kama yenye uwezo wa
kusababisha saratani ya ubongo mbali na athari nyinginezo hatari kwa
mwili kiafya.
Kwa mfano, watumjai wa Iphone, je mlijua kama
mnapaswa kuzibeba simu zenu umbali wa milimita 10 kutoka kwa mwili wako
kuhakikisha kuwa madini hayo hayaathiri mwili?
Licha ya kwamba
utafiti mpya unahitajika kuthibitisha hili....ni wazi kwamba madini
fulani yanayotumika kutengeza simu yanaweza kusababisha aina ya saratani
za mwilini.
Na ndio maana kampuni ya Belly Armor ikaja na wazo la
kuwatengezea wanaume nguo za ndani zinazoweza kuwakinga kutokana na
athari hizo.
KUTOKA http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/12/141212_belly_armor_brief
No comments:
Post a Comment