Monday 29 December 2014

DALILI NA MADHARA YA UGONJWA WA KISONONO


Mara nyingi ugonjwa wa kisosnono huwa hauonyeshi dalili yoyote mwanzoni. Lakini ukionyesha dalili basi kwa mwanaume utasikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuambatana na usaha kutoka uumeni, kwa mwanamke pia dalili ni hizo hizo - maumivu wakati wa haja ndogo na kutoa usaha ukeni.


Usaha huo unaotoka uumeni au ukeni, huwa mzito na rangi ya kijani-njano, ambapo kwa mwanaume anaweza kuhisi maumivu katika korodani zake.
Kwa Wanawake maumivu yanaweza  kuwa chini ya tumbo, uchungu wakati wa ngono, na damu Isiyokuwa ya kawaida kutoka kwenye uke.

 Kama kisonono huenda kikakaa kwa muda mrefu mwilini  bila kutibiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi ya afya. Katika wanaume, inaweza kusababisha makovu ndani ya njia ya mkojo, ambayo inaweza kusababisha maumivu wakati wa kukojoa. 

Katika wanawake, kisonono kinaweza kusababisha zaidi kutoka eneo la uke na kusababisha papo hapo ugonjwa mwingine wa "pelvic inflammatory" (PID) - maambukizi katika maeneo mbali mbali ya uzazi yanaweza kusababisha utasa.
 
Katika wanaume na wanawake, kisonono  kisichotibika kwa muda muafaka, huenda huweza kuenea kupitia damu katika sehemu za mwili ambazo ni mbali na viungo vya uzazi, na kusababisha uvimbe katika viungo, ngozi, mifupa, tendons, moyo, au hata eneo karibu na ini.

No comments:

Post a Comment

.