Homa ya Typhoid ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na bacteria Salmonella typhi
Ni homa inayoanza taratibu na joto la mwili kupanda hadi nyuzi joto 40C,kutokwa jasho,kuharisha na mara
chache kuharisha kulikochanganyika na damu. Inasambazwa kwa kula au
kunywa chakula au maji ambayo yamechafuliwa na kinyesi au mkojo wa mtu
mwenye maambukizi ya Typhoid
DALILI
Kuumwa kichwa kupita kiasi
Mwili kuchoka
Kukosa hamu ya kula
Maumivu ya Mwili
Kutokwa na damu puani
Kikohozi kikavu
Joto la mwili kuongezeka sana
Maumivu ya tumbo na kuongezeka ukubwa
Bandama kuongezeka ukubwa.
Tumbo kutoboka na kuvuja damu baada ya wiki 2 mpaka 3 za ugonjwa huu.
MATIBABU
Tyfoid ispotibiwa husababisha sana vifo kutokana na kutokana na kutoboa
tumbo na utumbo, kupoteza damu nyingi, na maambukizi mengine
yanayoendana na ugomjwa huu. Ugonjwa huu hutitibiwa kwa mchanganyiko wa
dawa kama Ciprofloxacin, chloramphenicol, trimethoprim-sulfamethoxazole, Amoxicillin Ceftriaxone na ampicillin sindano au vidonge kwa maelekezo ya daktari.
No comments:
Post a Comment