Tatizo la kutofanikiwa kupata ujauzito kwa mwanamke linahusiana moja kwa moja na kuwepo na tatizo kwa mwanaume.
Unaweza
kusema kama una tatizo hili endapo unaishi katika mahusiano ya kutafuta
ujauzito kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mafanikio.
Ili
mwanamke apate mimba ni lazima awe na sifa za kupata ujauzito, na ili
mwanaume aweze kumpa mwanamke mimba ni lazima awe na sifa za kumpa
mwanamke mimba.
Matatizo haya yapo kwa pande zote mbili.
Wakati
wa kutafuta ujauzito, ni vema mwanamke na mwanaume washirikiane kwani
mwanaume unaweza kujiona huna tatizo kumbe ukija kupima mbengu zako
utajikuta unatatizo kubwa.
Matatizo kwa mwanamke
Mwanamke mwenye tatizo la kutopata ujauzito anaweza kuwa na mojawapo ya matatizo haya yafuatayo;
Atakuwa
amekaa na mume au yupo katika mahusiano ya kutafuta mtoto kwa zaidi ya
mwaka lakini hakuna mafanikio, hulalamika maumivu ya chini ya tumbo mara
kwa mara au yanaweza yasiwepo, maumivu ya hedhi, kuvurugika mzunguko na
kutoona ute wa uzazi.
Wengine hawana hamu ya tendo la ndoa au
kutojihisi raha wakati wa tendo, maumivu wakati wa tendo au kutokwa na
uchafu ukeni wakati mwingine huambatana na muwasho na harufu.
Anakuwa
na historia aidha ya kutumia njia za uzazi wa mpango, kuharibu au kutoa
mimba, historia ya kuzaa, au kufanyiwa upasuaji wa aidha uzazi au
mirija. Ingawa wengine hawana historia hizi.
Nini cha kufanya?
Endapo
utahisi una matatizo ya kutopata ujauzito na unazodalili kama hizo hapo
juu au huna, basi ni vizuri umuone daktari wa magonjwa ya matatizo ya
uzazi katika hospitali za mikoa. Uchunguzi utafanyika kuangalia mfumo
wako wa homoni au vichocheo vya uzazi, vipimo vya kizazi na mirija na
vingine ambavyo daktari atashauri.
Uchunguzi na matibabu huchukua muda mrefu, ni vema kufuatilia kwa makini.
Athari kubwa zinazotokea mara nyingi katika uzazi kwa mwanamke ni kuziba kwa mirija ya mayai.
Mvurugiko wa mfumo wa homoni, matatizo ndani ya kizazi ambayo yanaweza kuwa uvimbe au maambukizi.
Uwezekano wa kutibiwa na kufanikiwa upo endapo utazingatia.
Matatizo ya uzazi kwa mwanaume
Mwanaume
kama atazingatia uchunguzi na tiba naye anaweza kufanikiwa ingawa
akigundulika kama anatatizo tiba yake huchukua muda mrefu.
Uchunguzi wa mwanaume ni kuangalia mbegu za uzazi na kupima korodani.
Mwanaume
unaweza kujifahamu kama unatatizo endapo utakuwa na dalili zifuatazo;
siyo lazima zote lakini mojawapo, upungufu wa nguvu za kiume,
kuishi
na mwanamke zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mimba, kutoa manii
nyepesi sana na zenye harufu mbaya, manii nyepesi hutoka mara moja ukeni
unapomaliza tu tendo la ndoa.
Maumivu ya muda mrefu ya korodani,
maumivu ya kiuno, maambukizi ya mkojo ya mara kwa mara, uvutaji wa
sigara kwa muda mrefu, unywaji wa pombe kali, na matumizi ya madawa ya
kulevya mfano bangi na mirungi na mengineyo.
Nini cha kufanya?
Matatizo
haya hutibika kwa daktari wa matatizo ya uzazi kwenye hospitali za
mikoa. Vipimo vya mbegu za uzazi vitafanyika kuangalia kiwango cha mbegu
na ubora wake kama zina uwezo wa kutungisha mimba.
Vipimo
vingine itategemea na uwepo wa matatizo mengine ya uzazi kwa mwanaume
kama kuwahi kumaliza tendo la ndoa, kushindwa kufanya tendo la ndoa,
upungufu wa nguvu za kiume, uchovu mkali baada ya tendo la ndoa, maumivu
ya kiuno, korodani na maumivu ya njia ya mkojo.
Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.
No comments:
Post a Comment