Tuesday, 9 December 2014

MTAALAMU WA UTAFITI ALIYEMEMEZWA NA NYOKA AINA YA ANACONDA

Watu nchini Marekani wameelezea ghadhabu na hasira zao kwenye mitandao ya kijamii kufuatia utafiti wa mtaalamu wa wanyamapori Paul Roslie kumezwa na Nyoka aina ya Anaconda ili ku chunguza maumbile ya ndani ya Nyoka huyo.

Lengo la utafiti huo ambao ulikuwa wa kwanza wa aina yake duniani, ilikuwa ni kuchunguza maumbulie ya ndani ya Nyoka huyo anayepatikana katika msitu wa Amazon.
Hata hivyo inaarifiwa bwana Paul alilazimika kusitisha utafiti wake ambao umezua utata muda mfupi tu baada ya kuuanzisha.
Watu nchini Marekani walijionea kwenye televisheni zao kipindi kilichokuwa kinapeperushwa cha mtaalamu huyo kuingia ndani ya tumbo la Anaconda akiwa amevalia vazi maalum ambalo yangesaidia kuchunguza kiwango cha joto mwilini mwake na pia kupima mipigo ya Moyo wake wakati akiwa ndani ya tumbo la Nyoka 
SOMA ZAIDI KUTOKA BBC SWAHILI.

No comments:

Post a Comment

.