Tuesday 30 December 2014

OGOPA SANA UNENE UNAWEZA KUKUPELEKEA MATATIZO HAYA.

Zifuatazo ni sababu 18 zinazokulazimu upunguze uzito wako na uogope unene. 1. Unene unaongeza kiwango cha mafuta mwilini, ambayo huongeza uwezekano wa kupata kensa.
2. Unene unaongeza mafuta mwilini, ambayo hufanya matibabu ya kensa kuwa magumu zaidi.
3. Unene huongeza mafuta mwilini ambayo huushinikiza na kuubana moyo. 

 4. Mtu mnene huwa mvivu kufanya mazoezi, suala ambalo humuongezea zaidi unene.
5. Mafuta mengi mwilini yana madhara kwa ubongo.
6.Unene huathiri hata tabia na miamala ya mtu.
7. Unene huongeza uzito katika mifupa na viunga vya mifupa (bone joints).
8. Unene husababisha kibofu cha mkojo kibanwe suala linalosababisha matatizo mbalimbali ya mkojo.
9. Unene hupunguza uwezo wa kujamiiana wa mtu.
10. Unene hupunguza uwezo wa kuzaa na hata kusababisha utasa na ugumba.
11. Unene hupelekea mwili upatwe kwa wepesi na magonjwa mbalimbali kama vile kisukari na presha.

12. Watu wanene wanapofika hospitalini upimaji wao pia huwa wa matatizo.
13. Unene husababisha ujauzito kuwa wenye matitizo mengi.
14. Unene huathiri pia afya ya mtoto mchanga anayezaliwa.
15. Unene hufanya matibabu ya asthma yawe magumu.
16. Unene hupelekea mtu asilale vizuri, na wakati mwingine mtu mnene anapolala hubanwa na pumzi suala linalomfanya aamke mara kwa mara.
17. Unene humfanya mtu ashindwe kuwajibika vizuri kazini, na hata kuathiri utendaji kazi wake.

18. Unene hufanya matumizi ya fedha kuwa makubwa.

No comments:

Post a Comment

.