Friday, 31 October 2014

MBINU ZA KUMFANYA MTOTO WAKO APENDE KULA.

Kutatua tatizo huanzia kwenye kujua tatizo liko wapi. Ushauri nasaha unaotolewa na madaktari ni kuwa, hakuna muarobaini wa kutibu hii tabia, bali ni swala la kujaribu mbinu mbalimbali ili kuweza kujua kitu kimoja kinachoweza kuwa suluhisho la ukataaji wa kula wa mtoto.
Katika njia muhimu alizopendekeza ni pamoja na hizi hapa:

1. Kubadilisha vyombo vya chakula vya mtoto

Mtoto huvutiwa zaidi na rangi, hasa kwenye vitu anavyotaka kula. Mtoto anaweza kuchoka kula chakula sababu anatumia chombo kimoja kila siku, hii haijalishi kama chakula kinabadilika au la. Ni muhimu kumuandalia mtoto chakula kwenye vyombo vyenye rangi na maumbo tofauti. Na ushauri wa daktari ni kuwa, usirudie chombo kwa wiki nzima, kama inawezekana. Hii inamfanya mtoto kuona utofauti wakati wa kula, na kumfanya apate hamu ya kula.
Mfano, unaweza kutumia bakuli, vikombe, sahani, vijiko vyenye rangi tofauti ili kumfanya aone anakula katika mazingira tofauti na hii humfanya awe na hamu kula chakula zaidi.

2. Watoto wale pamoja na familia


Watoto hupenda kuiga wazazi. Mara nyingi sana watoto hupewa vyakula wale wakiwa wenyewe wakati watu wengine wanaendelea na shughuli za kawaida. Hii inaweza kumfanya mtoto kupendelea zaidi kucheza kuliko kula. Ni muhimu kumlisha mtoto wakati familia nzima imekaa mezani au jamvini tayari kwa kula. Katika muda huu mtoto atakula vizuri bila vikwazo, maana kila mmoja anakula.
Vilevile, watoto wengine (umri wa miezi 10 hadi miaka 2) hupendelea kula vyakula wanavyokula watu wazima, hata kama haviwafai, na kugoma vyakula vya watoto. Ni bora kumuandalia chakula kinachofanana na unachokula wewe na kumpa ili apate kufurahia. Huwezi kubishana na mtoto, ingawa huwezi kumpa kila kitu anachotaka pia. Ila jaribu kutumia mbinu tofauti ili apate kula na kuridhika. Afya yake ni bora kuliko kitu kingine kwenye maisha yake kwa muda huu.

3. Jaribu kumsoma mtoto anapenda nini


Kila mzazi ana jukumu la kumsoma mwanae anapendelea nini. Ili kuweza kumfanya mtoto ale vizuri, ni vyema kubadilisha vyakula kila wakati – siyo kila siku. Mara nyingi watoto huchukua muda kuzoea chakula, hivyo ni vizuri kumpa mtoto chakula kwa muda wa siku 2 hadi 3 na kumbadilishia na chakula kingine. Hii inasaidia mtoto kuonja ladha ya chakula. Anaweza kukipenda au kukichukia. Kama atakataa ladha ya chakula kipya, usikate tamaa, jaribu kumpa tena baada ya siku moja au mbili, unaweza kukuta akaipenda ladha na akala chakula bila tatizo.
Usikate tamaa kwenye kumpa mwanao upendo wako kama mzazi. Jaribu kila njia unayoweza na usife moyo. Watoto ni wagumu kuwaelewa na inachukua muda, lakini pale unapofikia hatua ya kujua anachopenda utakuwa umepata jibu zuri jinsi ya kuendelea kumlea mwanao.

4. Epuka kumpa vitu vitamu kati ya milo


Watoto wengi wanapenda kula vitu vidogo vidogo (pipi, biskuti, juisi, keki n.k.) kila mara. Hivi vitafunwa vinaweza kumfanya mtoto azibe njaa na kutokuwa na hamu ya kula chakula muda unapowadia. Ili kuzuia hii tabia, ni bora kuacha kumpa mtoto vitu vidogo vidogo kati ya milo ili kumfanya kuwa na hamu ya chakula muda unapowadia.
Mara nyingi inashauriwa kumlisha mtoto mara 4 hadi 5 kwa siku. Hii ni vizuri sababu mwili wa mtoto unakuwa unahitaji virutubisho vingi mara kwa mara kwa kusaidia kukua. Ni vizuri kumpa mtoto chakula bora kuliko kumjaza tumbo na vyakula vyenye sukazi zisizo na kazi mwilini.

5. Msikilize mtoto anachotaka


Mara nyingi mzazi au mlezi unaweza kudhani kuwa unajua zaidi kiwango cha chakula anachotakiwa kula mtoto kuliko hata mtoto mwenyewe. Hili linaweza kuwa tatizo kubwa litakalopelekea mzazi kumlazimisha mtoto kula chakula kingi kupita kiasi. Fahamu kuwa, watoto wanajua kiwango cha chakula kinachowatosha na wakati gani ni muafaka wa kula. Hivyo, itakuwa rahisi kwako kama ukimsikiliza mtoto anataka nini, kuliko kulazimisha kile unachotaka wewe. Hakuna mtoto anayeweza kuvumilia kukaa na njaa. Watoto wote huhitaji chakula ili kucheza na kufurahi na wenzao. Hivyo basi, pale anakuwa na njaa atasema, au kulia, na ndio muda muafaka wa kumpa chakula unachotaka.
Swala muhimu la kuzingatia ni kuwa, katika mazingira yeyote, usimlazimishe mtoto kula. Usimkabe. Kulazimisha mtoto kula ni kumjengea tabia ya kuchukia chakula. Na akishajenga tabia hii hawezi kuacha sababu atakuwa anahusisha chakula na adhabu. Hakuna mtu anayependa adhabu. Hivyo, watu wengi wanaopenda kulazimisha mtoto kula kwa kumkaba huwa wanajenga tatizo kubwa zaidi ya lile la kula tu.

Thursday, 30 October 2014

TAMBUA NA KUJITIBU MAPEMA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Upungufu wa mbegu za kiume uchangiwa na kurithi magonjwa mbalimbali yanayoathiri mirija ya uzazi,  korodani na upungufu wa hormoni ya kiume (testosterone), kuumia kwa korodani, joto na unene kupita kiasi, ukosefu wa lishe asa zenye zinc, selium na vitamin C na D, kuvaa nguo za kubana muda mrefu, uvutaji wa sigara unyaji wa pombe na matumizi ya madawa kupita kiasi, unene kupita kiasi, maambukizi ya zinaa kwa muda mrefu, msongo wa mawazo na athari za mazingira kama sumu na mionzi.
DALILI ZAKE
Kukosa hamu ya kufanya mapenzi
Kushindwa kusimamisha uume.
Kuvimba au kuuma kwa korodani
Kupungua kwa nywele za kiume asa ndevu, sharubu na nywele za kifuani.
Kukosa mtoto baada ya mwaka mmoja wa kufanya mapenzi bila kinga.
Kuota maziwa kama mwanamke.
TIBA YAKE
Kula LISHE BORA, yenye kiasi kikubwa cha nafaka na matunda.
Punguza msongo wa mawazo.
Epuka uvutaji wa sigara, pombe na madawa kupita kiasi
Punguza kasi ya kufanya mapenzi au kupiga punyeto
Epuka nguo zinazobana na kuweka korodani katika joto kali.
Tatizo likizidi nenda hosipitali kwa uchunguzi na tiba asa inayohusisha upasuaji, dawa na ushauri.
USIPITWE BOFYA HAPA NA LIKE PAGE YETU KWA USHAURI NA TIBA ZAIDI.

LISHE NA VIRUTUBISHO VINAVYOTOKANA NA KULA MAYAI.

Mayai yana kiwango kikubwa cha virutubisho na madini ambayo ni muhimu sana kwa afya yako.  Hivi ni baadhi ya virutubisho vinavyoweza kuujenga mwili wako asa unapokula yai walau wara chache kwa wiki;-

ITAMBUE MAPEMA SARATANI YA MATITI

Saratani ya matiti ikigundulika mapema kwa njia ya uchunguzi na vipimo inatibiwa kabisa. Ewe mama, dada, shangazi, bibi na hata wewe baba wahi mapema upate ushauri na uchunguzi wa kitaalamu ili usiathiriwe vibaya na ugonjwa huu mara uonapo dalili hizi.

ITAMBUE MAPEMA SARATANI YA MATITI


Saratani ya matiti ikigundulika mapema kwa njia ya uchunguzi na vipimo kabisa. Ewe mama, dada, shangazi, bibi na hata wewe baba wahi mapema upate ushauri na uchunguzi wa kitaalamu ili usiathiriwe vibaya na ugonjwa huu mara uonapo dalili hizi.
Uvimbe usio wa kawaida katika maziwa au kwapani
Matiti kutoa majimaji
Mabadiliko ya rangi ya ngozi kwenye matiti
Ziwa moja kuwa chini au kuwa kubwa kuliko lingine.
Chuchu kuingia ndai au kuwa na vipele.

4 THINGS MAKES A MAN TIRED OF A WOMAN

Men get easily tired of a relationship; sometimes it’s not because they want to but because their lady does things that live them frustrated. Women sometimes are unaware of the fact that certain characters they exhibit would only push their man off the relationship.

Wednesday, 29 October 2014

MAMBO AMBAYO WANAUME WENGI UANGALIA SANA KATIKA KUJENGA UHUSIANO

Wanawake wengi hulalamika kuwa wanaume ni watata kwenye mapenzi.
Hulaumu kwamba ni ngumu kubaini vitu ambavyo wanaume huhitaji kutoka kwa wanawake.
Wanadai kuwa wakati mwingine hujitahidi kadiri ya uwezo wao kuhakikisha wanawapa furaha lakini wanaume huwa hawana hata msisimko.
Hapa chini, nimekuandalia vitu ambavyo wanaume huhitaji kwa wanawake wao. Moja kwa moja, mambo yakienda chanya huwa ni zaidi ya chombezo na hupagawa.
MAPENZI (Love)
Siku zote wanaume huangalia mapenzi kwa wenzi wao.

Mara nyingi wanaume huwa wepesi kuonesha mapenzi kwa wanawake wao lakini ndani ya nafsi zao, hutegemea mambo mengi kama malipo (return) ya upendo waliotoa kabla.
Wanapenda, kwa hiyo nao huhitaji kupendwa ili waone mambo yanakwenda sawa.

Wanawake wengi huwa wanaficha hisia za kupenda, hili huwaumiza wenzi wao.
Onesha mabadiliko, muoneshe jinsi unavyoridhishwa na upendo wake kisha mtamkie kwamba kwake umefika, halafu thibitisha hilo kwa vitendo.
MVUTO (Attractiveness)
Wanaume huhitaji wapenzi wao wawe na mvuto. Hii inawezekana isiwe na maana kwa wanawake kwa kushindwa kutambua mvuto wao, unavyoweza kuwa kibwagizo murua cha mapenzi.
Vaa vizuri upendeze, hakikisha muda wote unakuwa nadhifu.

Muonekano wako ndiyo utamfanya mwenzi wako ajiamini popote.
Kwa hiyo, kupendeza kwako ni bonge la chombezo kwa mwenzio.
UAMINIFU (Trustful)
Wanaume hupenda wanawake wenye uaminifu wa asilimia 100.

Mwanaume huhitaji mwanamke ambaye muda wote atakuwepo kwa ajili yake kimapenzi, kubadilishana mawazo na kumshirikisha katika siri za maisha yake.
Bahati mbaya wapo wanawake wengi ambao hawana uaminifu hata chembe.
Hilo huwafanya wanaume kukosa imani kwa wapenzi wao.
Jiamini kisha uwe muaminifu.
Mfanye mpenzi wako asikutilie shaka ya aina yoyote kisha uone jinsi maisha yanavyoweza kusonga mbele.
FAMILIA (Family)
Wazo la kila mwanaume anapopata mwanamke, hufikiria ajenge naye familia haraka iwezekanavyo. Hivyo basi, huhitaji mwanamke ambaye yupo tayari kwa hilo.

Kitu ambacho huwakera wengi ni pale wanapokutana na mtu aliye na mawazo ya kurukaruka.
Kama umeshaolewa, muoneshe mumeo jinsi ulivyo fundi wa kuiweka familia pamoja.
Ukifanya hivyo, utakuwa umempatia, kwani hakuna jambo ambalo wanaume huwa hawapendi kama kuona familia inasambaratika.
UKARIMU (Kindness)
Wanaume huwa na matarajio ya kuwaona wanawake wao wakiwa wapole, waungwana na wakarimu. Jitazame na ujitengeneze kuwa hivyo ili umvutie mwenzi wako.

Ukorofi, ubishi na roho mbaya siyo sifa ya kike.
UCHESHI (Funny)
Wanaume hupenda wanawake wanaojua kucheka. Akiwa naye, wazungumze na wacheke. Wanaume huwachukia wanawake wanaopenda kununa. Kama una tabia hiyo, jirekebishe ili umkune mwenzi wako.

U-MWANAMKE (Femaleness)
Kwa kawaida, wanaume hupenda wanawake ambao wanajitambua kuwa wao ni wanawake.

Huwachukia wale wanaojipa sifa ya u-dume au wababe, wanaopenda kutoa amri.
Huhitaji wanawake wanaotimiza wajibu wao kama wanawake kulingana na jamii inavyotambua. Hupenda wanawake wanaojali, kujiheshimu na kadhalika.
Wale walevi hukosa sifa ya u-mwanamke ambayo wanaume huihitaji.
LIKE PAGE NA TUTUMIE TATIZO LOLOTE LA KIAFYA TUTAKUSAIDIA KULITATUA 

MADHARA YA KULALA NA NGUO ZA NDANI.

Madaktari na waalamu wa afya wanashauri kulala bila nguo za ndani wakati wa usiku ili kuwezesha viungo vya uzazi kupata hewa ya kutosha ili kuepuka maambukizi ya fangasi na kutoa harufu mbaya katika sehemu za siri. Kuvaa nguo za ndani wakati wa kulala usababisha kubana sehemu za siri na joto kupita kiasi ambayo usababisha joto kupita kiasi na unyevu na kuvutia ukuaji wa fangasi na bakteria kwa jinsia zote huku pia zikisababisha upungufu wa mbegu za kiume na harufu mbaya.

MAGONJWA KUMI HATARI USIYOPASWA KUPUUZA.

Mwili wa binadamu huwa na kinga kwa ajili ya kupambana na magonjwa mbalimbali, wakati mwingine kinga hizi hushindwa kufanya kazi kutokana na magonjwa ambayo ni hatari sana hivyo kuitaji tiba au msaada utakaokuwezesha kuishi na ugonjwa huo. Yafuatayo ni magonjwa kumi hatari usiyopaswa kupuuza katika maisha.

KUHUSU KIFO CHA RAISI WA ZAMBIA.

Sata II
Aliyekuwa rais wa Zambia Michael Sata amefariki usiku wa jana tarehe 28 Oktoba kutokana na ugonjwa ambao bado serikali ya nchi hiyo haijaweka wazi.

Tuesday, 28 October 2014

MADHARA YA KUTOBOA PUA, MDOMO NA ULIMI

Katika zama hizi za utandawazi na muingiliano baina ya tamaduni zetu za asili na tamaduni za kimagharibi, imekuwa ni kawaida kwa vijana wa rika tofauti na jinsia zote kutoga ulimi, mdomo, kitovu ama kivimbe cha nyusi kwa sababu tofauti tofauti sana. Hivyo basi, ni muhimu sana kufahama ukweli kuhusu faida ama hasara za kutoga ulimi ama mdomo kabla hujatekeleza azma yako ya kutoga viungo hivi vya mwili.


Kutoga Ulimi ama Mdomo kunaweza kukusababishia madhara yasiyotarajiwa
Matokeo mazuri zaidi ya kutoga ulimi ama mdomo ni kutokutokea kwa kidonda ama kivimbe, wakati matokeo mabaya kutokea kwa baadhi ya watu ni pamoja na kuvunjika kwa meno/jino, kuvuja kiasi kikubwa cha damu, ama maambukuzi ya bakteria kwenye kidonda. Kutoga ulimi hujumuisha kutumika kwa sindano inayopenyezwa katikati ulimi ili kupitisha na kuhifadhi kipini, ama ndoana ama hereni ya urembo. Kazi hii ya kutoga ulimi mara nyingi ganzi huwa haitumiki. Baada ya kutoga, kuvimba kwa ulimi na maumivu ya muda hutokea. Madhara ya kutoga Ulimi 
  • Kuvuja damu kiasi kidogo hutarajiwa, kuna hatari ya mishipa ya damu kuharibiwa wakati wa kutoga ulimi, hali inayoweza kusababisha kuvuja damu kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyotarajiwa.
  • Ingawa kuvimba kwa ulimi kunatarajiwa baada ya kitendo cha kutoga ulimi, wakati mwingine ulimi huvimba kwa kiasi cha kuziba kwa njia ya hewa. Kuziba kwa njia ya hewa kunaweza kusababisha kifo.
  • Ikiwa fundi wako wa kutoga ulimi hana uzoefu wa kutosha kufanya kazi hiyo, anaweza kuharibu mishipa ya fahamu ya ulimi hivyo kuharibu uwezo wa ulimi kuhisi/kutambua hisia za joto,baridi ama ladha ya chakula na vinyaji, vile vile kuathiri mienendo ya viungo vya eneo la kinywa na uso. Kwani nyuma ya ulimi kuna mishipa ya fahamu,mishipa hii ikiharibiwa ulimi utapooza hivyo kusababisha ganzi la kudumu, kuathirika kwa uwezo kuongea na kushindwa kutambua ladha za chakula/vinywaji
  • Vilevile kutoga ulimi kunakuweka kwenye hatari ya kupata maambukizi kwenye ulimi hasa ikiwa hutaweza kutunza hali ya usafi wa kinywa na meno kila wakati, hivyo kusababisha wadudu jamii ya bakteria kupenya na kuingia ndani ya ulimi na kusababisha maambuzi kwenye ulimi.
  • Hali ya kutoga ulimi inapodumu kwa muda mrefu, inaweza kusababisha nyufa kwenye meno, ama kuvunjika kwa nyuso za jino/meno kwa sababu ya msuguano wa muda mrefu kati ya jino/meno na hereni/kipini ama ndoana ya chuma/plastiki iliyohifadhiwa kwenye ulimi kwa muda mrefu. Nyufa hizi kwenye meno, kwa kawaida husababisha maumivu makali ya jino/meno. Hivyo basi meno haya yenye nyufa yanaweza kutibiwa kwa kuvalishwa kofia “ dental crown”. Si kawaida kupata magonjwa ya fizi ama kuta za ndani za shavu ikiwa umetoga ulimi na unatunza afya ya kinywa na meno vizuri.
Kutoga Mdomo
Kutoga mdomo ni pale pete ya urembo inapovalishwa ama kuhifadhiwa ndani ya mdomo. Majeraha ya kutoga mdomo hupona haraka zaidi, hata hivyo unapaswa kutunza kidonda cha jeraha hili kwa umakini
mkubwa wakati wa kupona. Vyakula, vinywaji na moshi wa sigara vinapofikia kidonda hiki, vinaongeza hatari ya kupata maambukizi kwenye kidonda.
Kishikizo vishikizo vya pete hii ya urembo kinaweza kusababisha vidonda kwenye fizi ama kuharibu jino. Kwa baadhi ya watu, tiba ya kupandikiza fizi hutumika kurejesha fizi zilizoathirika. Kama ilivyo kwa kutoga ulimi, kutoga mdomo pia kunaweza kuathiri mshipa wa fahamu hivyo kuathiri mienendo ya misuli ya kwenye eneo la kinywa na mdomo.
Je, una mpango wa kutoga Ulimi ama Mdomo?

Ikiwa unapanga kutoga viungo hivi vya mwili, unashauriwa ufanye mambo yafuatayo yatakayo kuwezesha kupata huduma ambayo haita athiri afya yako:


  • Hakikisha ngariba mtoga ulimi ama mdomo sio tu ana uzoefu wa kutosha kwenye kazi anayofanya, bali pia anazingatia usafi kufanya kazi zake.
  • Nenda hospitali kupata ushauri tiba mara tu unapoona ama maumivu ni makali sana, kuvimba kwa ulimi ama damu zinavuja kwa muda mrefu (zaidi ya dakika 30) ama ikiwa jeraha linapata maambukizi ya bakteria.
  • Unapokuwa na hereni, pete ama ndoana ya urembo kwenye ulimi ama mdomoni, unashauriwa kumwona daktari wa kinywa na meno kila baada ya miezi sita (6). Daktari wa meno atafanya kazi ya kuhakiki ikiwa kidude kilichovalishwa kina madhara kwenye meno ama fizi, hivyo kudhibiti athari zinazoweza kutokea kwa kutoga ulimi ama mdomo.
  • Wana michezo wanashauriwa kutovaa hereni, pete ama ndoana ya urembo iliyopo kwenye ulimi ama mdomoni wanapokuwa mchezoni, kwani vyombo hivi vya urembo vinaweza kunasa kwenye ngozi bila kutarajia hivyo kusababisha madhara yasiyotarajiwa
USIPITWE NA MENGI LIKE PAGE NA WASILIANA NASI FACEBOOK KWA MSAADA ZAIDI.

CHAI YA RANGI INAVYOSAIDIA KUZUIA SARATANI YA KIZAZI.

Hii ni habari njema kwa wanawake wanaopenda kunywa walau kikombe kimoja cha chai nyeusi na juisi ya machungwa kila siku vina virutubisho vya  flavonols and flavanones ambavyo upunguza na kuzuia vifo vinavyotokana na saratani ya kizazi kwa wanawake asa wenye umri zaidi ya miaka 50.

MAMBO MUHIMU AMBAYO WANAWAKE HUVUTIWA KWA WANAUME.

Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.

VYAKULA VINAVYOFAA KWA WANAUME

1. Chokolate, hurekebisha mzunguko wa damu na kuondoa mafuta ambayo hayafai kwenye mishipa ya damu hivyo kukuepusha na shinikizo la damu. Ila kula mara kwa mara itasababisha kuongezeka uzito.

MUUGUZI KUISHITAKI SERIKALI BAADA YA KUWEKWA KARANTINI YA EBOLA

Siku chache baada ya New York na New Jersey kutangaza utaratibu mpya wa kuwaweka karantini wauguzi na madaktari waliotoka kuhudumia wagonjwa katika nchi zilizoathiriwa na Ebola, muuguzi wa kwanza kuathiriwa na utaratibu huo Kaci Hickox ametishia kufungua mashtaka kutokana na kufanyiwa kitendo hicho.

SOMA TAARIFA MUHIMU KUTOKA DAWASCO.


Sunday, 26 October 2014

DALILI KUMI ZA MALARIA AMBAZO HUPASWI KUPUUZA.

1. Homa kali
2. maumivu kwenye viungo na mgongo,
3. kichefuchefu,
4. kutapika,
5. kuharisha,
6. maumivu ya kichwa,
7. kutokwa jasho nyakati tofauti,
8. kizunguzungu,
9. degedege hasa kwa watoto wadogo.

10. kupoteza fahamu.

JE…UNAFAHAMU KUHUSU TETEKUWANGA (CHICKENPOX) ??

Ni ugonjwa wa ngozi unaotokea hasa wakati wa utoto na unasababishwa na kirusi aina ya varicella-zoster

Watu hupata ugonjwa huu Zaidi katika umri wa miaka 15,na wengi Zaidi kati ya miaka 5 hadi 9,ingawa katika umri wowote unaweza ukapata matetekuwanga

Ni ugonjwa unaoambukizwa kwa urahisi Zaidi.

VYANZO VYA UGONJWA WA U.T.I KWA WANAWAKE.

Vyanzo vinavyosababisha ugonjwa wa UTI ni matumizi ya maji  machafu wakati wa kujisafisha au kuoga ambayo huweza kuweka bakteria kwa urahisi na mwanamke kupata UTI.
Uchafu wa vyoo ni sababu nyingine asa matumizi ya vyoo ambavyo ni vichafu. Chooni kuna bakteria wengi ambao wanaweza kusababisha UTI.

Saturday, 25 October 2014

TIBA KWA WANAOTOA HARUFU MBAYA MDOMONI

Harufu mbaya ya mdomo husababishwa na kutofanya usafi  pamoja na maambukizi sehemu  mbalimbali za mdomoni au kwenye njia ya hewa  Ili huweze kupunguza na kuzuia hali hiyo fanya yafuatayo:

Friday, 24 October 2014

KUHUSU DAKTARI ALIYEPATIKANA NA VIRUSI VYA EBOLA.




JINSI YA KUTAMBUA NA KUDHIBITI UGONJWA WA PRESHA MAPEMA.

Presha ya Juu hutokea endapo itazidi kiasi cha140/90mmlHg na ikiwa haitibiwi huharibu mishipa ya damu katika macho, misuli ya moyo kuwa minene , kusababisha mshutuko wa  moyo (heart attack), mshipa ya damu safi kuwa migumu, figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure) na kiharusi (stroke).  Presha kwa mwanamke mjamzito inaweza kusababisha kifafa cha mimba na kufanya hata kiumbe kufa tumboni. Hivyo ni muhimu kuchunguza presha ya wanawake wote wajawazito.

KUPONA VIDONDA VYA TUMBO FUATA MAMBO HAYA MUHIMU SANA.

Watu wengi wamekuwa wakilalamika kutopona vidonda vya tumbo baada ya kutumia dawa mbalimbali sababu wamekuwa wakipatiwa dawa ambazo hazitibu kabisa tatizo hilo bali kupunguza maumivu.Baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu sasa suluhisho la tatizo hilo limepatikana na hakuna tena sababu ya kuishi na vidonda vya tumbo. Unaweza kupona Vidonda vya tumbo amabvyo hupatikana kwenye utumbo mdogo (duodenal alcer) na vidonda kwenye tumbo(Gastric ulcers) endepo utafuata mashariti ya fuatayo:

ZITAMBUE HASARA ZA KUZAMA CHUMVINI.

Tafiti zimeonyesha kuwa,mdomo wa binadamu ki bacteriologia (bacteriologically) ni mchafu maradufu kuliko sehemu ya uke(vagina).
Ni vema kufahamu kuwa,katika hali ya afya,binadamu wote tunaishi na vimelea(microorganisms) katika sehemu nmbalimbali za miili yetu, wakiwa na lengo la kutulinda, kitaalamu wanaita normal flora hawa wanakuwa hawana madhara katika mwili.Hivyo ni kweli kuwa vagina kama ilivyo mdomo una normal flora.
sasa baadha ya vitendo huweza kuondoa normal flora na kukaribisha magonjwa,mfano kinamama kujiosha ukeni na maji ya ndimu,limao,Shabu etc huweza kuondoa Normal flora na kukaribisha magonjwa,kama ambavyo matumizi ya sabuni zenye kemikali zinavoweza kuua normal flora kwenye ngozi na kusababusha magonjwa ya ngozi.Hivyo kwa mwanamke mwenye afya,uke ni mahali salama kufanya upendalo(kama vile kwenda chumvini).
Hata hivyo, nionye kuwa hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa kinywani kama vile Gonnorhea, Syphilis, candidiasis (fungus), HIV n.k ipo pale pale kama ambavyo mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya kawaida ya kujamiiana.
Mwisho, kama wewe ni mgonjwa wa kwenda chumvini, hakikisha unafanya mchezo huo nampenzi/mke aliye salama.

MAUMIVU NA KUVIMBA KATIKA SEHEMU ZA HAJA KUBWA

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri

Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.


Ndani
: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.


Je bawasiri husababishwa na nini?

Bawasiri husababishwa na;



  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu na kinyesi wakati mwengine kutokwa damu kisha ndio kupata kinyesi
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa


Dalili za bawasiri


  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa


Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri


  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids





Vipimo na uchunguzi



  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)


Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri


  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy



Njia za kuzuia Bawasiri


  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji ya Uvuguvugu mengi kwa siku (glasi sita hadi nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.



Kutibu kwa kutumia njia Mbadala Maradhi ya BAWASIRI:




Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine

TIBA 1:
MAKAL-ARZAK


Chukua 100grm kwa kila lita moja na robo ya maji (1250ml).


Chemsha mpaka ibakie lita moja kamili.

Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha kahawa (50ml) kutwa mara tatu (1×3) mpaka dawa imalizike.

MWIKO
: Mgonjwa asitumie nyama nyekundu aina yoyote,asile pili pili na wala asitumie vitu vikali.Badala yake atumie kwa wingi mboga za majani,matunda,maziwa na samaki.


TIBA 2:

Changanya unga wa Habat soda na Asali safi ya nyuki vipimo vya sawa kwa sawa.Halafu kunywa kijiko kimoja kimoja mara kwa mara.Fuatilishia na kumywa maji glasi moja (250ml) kila umalizapo kunywa hiyo dawa.

TIBA 3:

Jipake mafuta ya Mbarika kwenye utupu wa nyuma ambapo ndipo bawasiri hutokea.Fanya hivyo mara kwa mara, kwa sababu huirudisha hiyo bawasiri ndani.

HALI NI MBAYA KATIKA HOSIPITALI YA OCEAN ROAD.

Hali ni mbaya katika hospitali ya Ocean Raod Dar es salaam kutokana na uhaba mkubwa wa dawa.
Wagonjwa wengi waliolazwa katika hospitali hiyo kwa nyakati tofauti wamesema wameshuhudia wenzao kadhaa wakipoteza maisha kwa kuwa taasisi hiyo haina dawa za kuwatibu.

MWANAMKE AFARIKI AKIFANYIWA UPASUAJI WA MAUMBILIE.

Mwanamke mmoja amefariki wakati akifanyiwa upasuaji wa kurekebisha maumbile.
Mwanamke huyo raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 amefariki nchini Thailand alikokwenda kufanyiwa upasuaji huo, ambapo taarifa kutoka nchini humo zinasema baada ya kupatiwa vidonge vya usingizi mapigo yake ya moyo yalisimama.
Taarifa kutoka Thailand zinasema upasuaji huo ni wa awamu ya pili kufanyiwa, baada ya kutoridhiwa na matokeo ya upasuaji wa awali.

Thursday, 23 October 2014

HIZI NI FAIDA ZA BIZARI KIAFYA KATIKA MBOGA.

Bizari, almaarufu kama kiungo cha chakula, ina ladha ya pilipili na harufu kali kiasi kwa kunusa. Ni mojawapo ya viungo muhimu kwenye chakula, hasa pilau. Bizari inatokana na mizizi, ni jamii ya tangawizi.
Bizari hutumika katika kutengeneza curry na haradali (mustard), na ndio huifanya haradali kuwa na rangi yake ya manjano.

FAIDA NA JINSI YA KUPANGA RATIBA YA CHAKULA KWA AFYA YAKO.

Ili kuwa na siha njema ni muhimu kula vizuri. Kula vizuri si rahisi, ingawa wengi wetu tunadhani kula vizuri ni kula chakula tunachokipenda – chips, kuku, mayai, nyama na vingine. Hii ni kasumba mbovu tu. Kula vizuri (au balanced diet) si lazima kula vyakula unavyopenda, bali kula vyakula vyenye afya na kujenga mwili wako. Njia moja mbadala ya kuhakikiasha unakula vizuri na kwa afya ni kuwa na ratiba ya wiki ya chakula. Leo tunaangalia umuhimu wa kupanga ratiba ya chakula kwa afya yako na familia yako.

VYAKULA VINAVYOFAA KWA WATOTO WENYE UMRI WA MIEZI SITA

Mara nyingi tumekuwa tukishauriwa kuwaanzishia watoto wetu chakula cha ziada tofauti na mziwa ya mama pale wanapofikisha umri wa miezi sita kwa ajili ya ukuaji mzuri. Vyakula unavyoshauriwa kumpa mtoto wako katika kipindi hiki ni vile vyenye uwezo wa kumeng'enywa kirahisi, virutubisho vya kutosha pamoja na kiasi kidogo cha chumvi na sukari kwani huweza kusababisha madhara afya ya kibofu na meno.

UGONJWA WA MABUSHA, DALILI ZAKE, ATHALI ZAKE NA TIBA YAKE

Mabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu. Hali hii hutokea kunapokuwa na
mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani. Kwa hapa nchini,
tatizo hili ni maarufu sana maeneo ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kiasi cha kuhusishwa na imani kadhaa kama unywaji wa maji ya madafu. Aidha, tatizo hili limekuwa likichukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni hali ya kudhalilisha ingawa kwa wengine huonekana ni hali ya kuwa ‘mzee wa heshima’ au ‘umwinyi’.

MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria. Unaweza kufanya yafuatayo ili kuepuka swala la chunusi usoni ambalo uharibu urembo wa ngozi yako.
1.    Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.

2.  Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
 
3.  Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)

4.  Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.

5.  Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.

6.  Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D

7.  Punguza mawazo 
8. Pia unaweza kupaka mask za asali, mayai, sabuni na asali kwa muda wa masaa 4 ili kusaidia ngozi yako kuwa laini.

Wednesday, 22 October 2014

CHANJO YA EBOLA KUANZA KUTUMIKA JANUARY 2015: WHO

Naibu Mkurugenzi  wa Shirika la Afya Duniani - WHO - Dr. Marie Paule Kieny alisema Jumanne majaribio ya dawa ya chanjo ya Ebola yanaendelea huko Ulaya  Marekani na Afrika, na kwamba kama chanjo hizo zikionekana kuwa salama kunaweza kuwa na majaribio Afrika magharibi mwezi Januari , wakitumia maelfu kwa maelfu ya dozi.
Akiongea na waandishi huko Geneva Dr. Kieny hakusema ni lini chanjo ya Ebola inaweza kupatikana duniani kote.
Hakuna dawa wala chanjo ya ugonjwa huo ambao umeuwa zaidi ya watu 4,500 huko Afrika Magharibi mwaka huu.
Jumatatu WHO ilitangaza taifa la Nigeria kuwa halina tena ugonjwa wa Ebola baada ya siku 42 kupita bila ripoti za kesi mpya a ugonjwa huo.

Tuesday, 21 October 2014

NAFASI ZA KAZI KUTOKA JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI(EAC)

BOFYA HAPA KUSOMA NAFASI ZOTE

MAMBO NANE YANAYOKUWEKA KATIKA HATARI YA KUUGUA UGONJWA WA KISUKARI

Yafuatayo ni mambo 8 yanayoweza kukuweka katika hatari ya kuugua ugonjwa wa kisukari.

KUHUSU MCHEZAJI ALIYEFIA UWANJANI AKISHANGILIA BAO

Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala 23 amefariki kutokana na majeraha ya uti wa mgongo aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea goli alilosawazisha  dhidi ya Chanmari West FC. Mchezaji huyu akifariki muda mfupi baada ya kukimbizwa hosipitali na kufanyiwa upasuaji. 

MAAJABU YA NDEGE KUGEUKA MTU NA KUANGUSHIWA KICHAPO HADI KUFA NIGERIA

Kisa cha kushangaza kilitokea nchini Nigeria ambapo mwanamke mmoja alipewa kichapo cha mbwa hadi akafariki kwa madai ya yeye kuwa mchawi.
Mwanamke huyo inasemekana alikuwa Ndege iliyokuwa inaruka mtini kabla ya kugeuka na kuwa binadamu.

Monday, 20 October 2014

NJIA RAISI ZA KUHESABU SIKU ZAKO ILI KUEPUKA MIMBA ZISIZOTARAJIWA



1. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd.
Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake. Hivo 8th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!


2. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 14th day. Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 28. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!


3. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:

1st
, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 21st day. Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 35. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!


4. Kama mwanamke ana abnormal menstration cycle ya siku 15 , BASI KUNAUWEZEKANO WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:

Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama kawaida:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 1st day. Inamaana kwamba, the 1st day of her bleedind ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 15. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa kundi hili anaweza kupata mimba!

Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa. Mwanamke wa aina hii anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linakuwa tayari kurutubishwa!

Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed. Pia wanawake wa kundi hili huwa wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu; na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu!

Jambo la kushangaza ni kwamba, wanawake wengi hawana knowledge ya kutosha juu ya hili suala la siku ya mimba; hasa wale ambao wana menstration cycle inayobadilikabadilika! Wao husitukia tu wameanza ku-bleed. Ndo maana hawawezi hata ku-plan kutopata mimba! Hawana ujanja kabisa ndio sababu wengi wanatumia sindano na njia zingine nyingi za artificial ambazo mwisho wa siku huwaletea matatizo ya uzazi, kwani nyingi hu-block njia ya uzazi! Nimeona wengi wenye matatizo ya uzazi unaosababishwa na hizi artificial family planning. Wengine hulazimika kwenda hospital kuzibuliwa ili wapate mimba jambo ambalo ni hatari kwa afya zao!

.