Baadhi ya tabia zetu ambazo wengi huzifanya pasipo kuyajua
madhara yake na kujikuta zikituharibia ama kuua ubongo au maini ambazo
ni sehemu muhimu mwilini mwetu.
Wednesday, 27 August 2014
Tuesday, 26 August 2014
DAKTARI AFARIKI KWA EBOLA
Daktari mmoja kutoka Liberia ambaye aliambukizwa ugonjwa wa Ebola na kutibiwa na dawa ya ZMAPP ameaga dunia.
Waziri mmoja wa Liberia alisema kuwa dakta
Abraham Borbor aliyekuwa miongoni mwa madaktari 3 waliopewa dawa hiyo
ambayo haijafanyiwa majaribio aliaga dunia mapema leo .
ZMapp iligonga vichwa vya habari iliposaidia madaktari wawili kutoka marekani kupata afueni kutokana na makali ya Ebola .
TAKWIMU ZINAONYESHA EBOLA INASAMBAA KWA KASI
Huu ni choro unaoonyesha takwimu jinsi Ebola inavyosambaa kwa kasi mwaka huu kuazi vilipogundulia virusi vyake mwaka 1976 katika mto Ebola nchini DR Congo.
MAMBO YA KUFANYA KILA UAMKAPO ASUBUHI
Kwa kawaida mida ya asubuhi huwa ni rafiki mkubwa kwa binadamu kwani uamka ukiwa na akili mpya ili kuanza siku mpya. Haya ni mambo ambayo unapaswa kufanya pale uamkapo asubuhi ili kuboresha afya yako kwa kuepuka magonjwa ya moyo, akili, na kupata mafanikio katika maisha.
MADHARA YA VIATU VIREFU NA JINSI YA KUEPUKA
Mchuchumio’ ama viatu vyenye visigino virefu, ni mojawapo ya
vitu vinavyopendwa na baadhi ya wanawake mbalimbali, sio Tanzania pekee
bali dunia nzima.
Wataalamu wanaeleza kuwa viatu hivi huharibu pingili za uti wa mgongo na huvunjavunja mifupa ya visigino. Wanawake wenye maumbo ya kati, ambao si wanene wala wembamba wamekuwa wakipendelea viatu virefu. Kwa kiasi kikubwa wasichana wafupi, wamekuwa wakipendelea kuvaa viatu virefu ili angalau na wao waonekane warefu.
Monday, 25 August 2014
MIGUU KUUMA KUTOKANA NA UMRI
Mwili wa binadamu ni kama mashine umri unavyozidi kwenda basi viungo navyo vinachoka. kutokana na uzito maumivua haya uanzia kwenye miguu kutokana na kuvimba na kujaa maji kwenye jointi au kukosa vilainisha. Hali hii usababisha maumivu makali kwenye misuli, mifupa, jointi, mwili kuwa dhaifu, kukosa usingizi na kushindwa kutembea.
Saturday, 23 August 2014
TATIZO LA KUUMA NA KUSAGA MENO KWA WATOTO WADOGO.
Watafiti wengi wameshindwa kubainisha dhahiri nini usababisha mtu kutafuna au kuuma meno usiku ili inahusishwa sana na minyoo, maambukizi katika meno na masikio, hasira na msongo wa mawazo kwa yaliyotokea siku nzima, mgangilio mbovu wa meno.
MAKOSA YANAYOFANYWA NA WANAWAKE WENGI KWENYE CHUMBA CHA DAKTARI
Haya ni makosa ambayo wasichana na wanawake wengi huyafanya mara nyingi wanapokuwa katika chumba cha daktari na hivyo kusabbisha ugumu kwa matibabu yao. Yasome kwa makini kama ushawahi kuyafanya au kukutana nayo yaepuke.
Friday, 22 August 2014
FAIDA YA MTOTO KULIA ANAPOZALIWA
Faida ya mtoto kulia anapozaliwa ni kufungua njia yake ya hewa (respiratory pathway) pale anapokutana na mazingira ya nje yenye ubaridi tofauti na tumboni. Hii usaidia kufanya exchange ya oxygen na carbon dioxide kwenye mapafu
kuanza kufanyika. Asipolia inamaana kuna uwezekanano wa kuhathiriwa na carbon dioxide
nyingi sana kwenye damu na kusababisha chembe hai za kwenye ubongo
(brain cells) kukosa hewa (hypoxia) na hii husababisha hizo cells zife
matokeo yake mtoto anaweza kupata utaahira (cerebral palsy) au kifo.
Thursday, 21 August 2014
TATIZO LA MIGUU NA MIKONO KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI.
Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na
hivyo kupoteza uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuAatayo:
- Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B,(Vitamin B Complex).
- Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi
- Uzito mkubwa wa mwili.
- Ugonjwa wa kisukari(diabetic neuropathy).
- Shinikizo la damu.
- Unywaji wapombe kupita kiasi
- Magonjwa ya figo.
MAMBO YA KUFANYA ILI KUFURAHIA TENDO LA NDOA.
Swala la mapenzi ni muhimu na kawaida kwa binadamu asa pale muda wake unapofika. Yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya ili kuongeza hamu, utamu na ashiki kwa mwenzako ili kumridhisha na kuboresha uhusiano.
Wednesday, 20 August 2014
JINSI YA KUJITIBU HARUFU MBAYA YA KWAPA.
Harufu ya kwapa haisababishwi na kutokwa na jasho bali bakiteria wanaovutiwa na jasho au unyevu chini ya kwapa. Hii umkosesha mtu ujasiri na kujiamini, au kuwa kero mbele za watu. Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo
VYAKULA VINAVYOFAA KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo husababishwa na bakiteria aina ya H. pylori ambao uishi kwenye tabaka za tumbo na utumbo mdogo. Kwa mtu ambaye ambaye ulinzi wa tabaka hizi uko sawa vimelea hawa uishi bila madhara yoyote wakati kwa wale ambao ulinzi umeharibiwa na dawa za aspirin, NSAID, saratani katika mfumo wa chakula, uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kali kupita kiasi uleta madhara ya vidonda vya tumbo kama maumivu makali juu ya tumbo na kuvimbiwa, kiungulia, kichefuchefu na kutapika. Endapo unasumbuliwa na tatizo ili unaweza fika hosipitali ambapo dawa za kuua bakiteria na kukomesha na kuzuia uzalishaji wa tindikali ambayo uharibu ukuta wa tumbo sambamba na kuepuka vyakula vinavyochochea uzalishaji wa tindikali hii unashauriwa kula vyakula vifuatavyo:-
Tuesday, 19 August 2014
TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI
Nyama za puani ni nyama laini zilizoota na kuning'inia kwenye njia ya hewa na mianzi ya pua ambazo husababiswa na uvimbe wa muda mrefu kwenye mfumo wa upumuaji, pumu, maambukizi ya mara kwa mara, aleji na magonjwa mengine ya njia ya hewa.
Nyama zikiwa ndogo huwa hakuna dalili wala ishara zozote zinazoingilia mfumo wa upumuaji ila zinapokuwa kubwa uzuia hewa kuingia na kuharibu mfumo wa upumuaji sambamba na kushindwa kunusa, maumivu ya uso, maumivu ya meno ya juu, mafua, kukoroma, macho kuwasha na maambukizi ya mara kwa mara katika njia ya hewa.
Nyama zikiwa ndogo huwa hakuna dalili wala ishara zozote zinazoingilia mfumo wa upumuaji ila zinapokuwa kubwa uzuia hewa kuingia na kuharibu mfumo wa upumuaji sambamba na kushindwa kunusa, maumivu ya uso, maumivu ya meno ya juu, mafua, kukoroma, macho kuwasha na maambukizi ya mara kwa mara katika njia ya hewa.
KWA WANAOSUMBULIWA NA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU.
Tatizo la kuvimba miguu husababishwa na kujikusanya kwa maji maji ambayo uvuja kutoka katika mishipa ya damu kutoka na sababu mbalimbali zinazosababisha damu ishindwe kurudi kwenye moyo kutoka katika miguu. Hali hii huweza kutokea pia kwenye mapafu, ubongo, tumboni, na kwenye mapaja lakini kutikana na mvuto wa dunia huweza kuonekana zaidi kwenye vifundo vya miguu na bila maumivu.
Mambo yanayochangia na kusababisha tatizo ili mara nyingi huwa ni ujauzito, ugonjwa sugu wa ini, figo, ini na moyo kushindwa kufanya kazi, dawa za kupunguza mfadhaiko na shinikizo la damu.
MATIBABU YAKE.
Mambo yanayochangia na kusababisha tatizo ili mara nyingi huwa ni ujauzito, ugonjwa sugu wa ini, figo, ini na moyo kushindwa kufanya kazi, dawa za kupunguza mfadhaiko na shinikizo la damu.
MATIBABU YAKE.
Fika hosipitali kama kuvimba miguu inaambatana na kubanwa na kifua, kushindwa kupumua, maumivu makali ya kifua, kuna uvimbe wenye maumivu au joto kali, matatizo ya moyo, ini na figo ambapo dawa za kupunguza majimaji mwilini, kusaidia moyo, ini na figo kufanya kazi zitatolewa kwa kwa maelezo ya wataalamu wa afya.
Unaweza kufanya yafuatayo kujitibu mwenye kabla ya kumuona daktari- Nyanyua miguu yako juu ya usawa wa moyo wakati umelala kwa muda wa dakika 30 ili kuwezesha damu ya kutosha kurudi kwenye moyo. Fanya hivi walau mara 3 kwa siku kupata matokeo bora zaidi
- Kufanya mazoezi laini pia itakusaidia kupeleka damu kwenye moyo na hivyo kurekebisha mzunguko wa damu
- Wakati unasafiri safari ndefu hakikisha unasimama mara kwa mara.
- Epuka kuvaa kwa muda mrefu nguo zinazobana sehemu za mapaja.
- Punguza uzito.
JINSI YA KUZUIA MAUMIVU WAKATI NA BAADA YA TENDO.
Maumivu haya wakati na baada ya tendo hutokea wakati wa tendo au baada ya tendo la ndoa na husababishwa na matatizo mengi katika njia ya uzazi. Kama maumivu yanatoka ndani kabisa ya nyonga huweza kusababishwa na maambukizi katika via vya uzazi(PID) na uvimbe.
Kuvimba au maambukizi ya njia ya mkojo(UTI) na Zinaa kama Chlamydia usababisha maumivu ndani ya uke na kwenye shingo ya kizazi. Majeraha na kuumia kwa sehemu za uke au uume usababisha maumivu sehemu za nje na ndani ya uke wakati na baada ya tendo.
Maumivu juu na katika ngozi ya sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya fangasi au vipele na makovu sehemu za siri.Kukosa maandalizi ya kutosha kabla ya tendo hufanya misuli ya uke kukaza kusababisha maumivu makali wakati na baada ya tendo.
Kuvimba au maambukizi ya njia ya mkojo(UTI) na Zinaa kama Chlamydia usababisha maumivu ndani ya uke na kwenye shingo ya kizazi. Majeraha na kuumia kwa sehemu za uke au uume usababisha maumivu sehemu za nje na ndani ya uke wakati na baada ya tendo.
Maumivu juu na katika ngozi ya sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya fangasi au vipele na makovu sehemu za siri.Kukosa maandalizi ya kutosha kabla ya tendo hufanya misuli ya uke kukaza kusababisha maumivu makali wakati na baada ya tendo.
Monday, 18 August 2014
JINSI YA KUMKINGA MWANAO NA POLIO
Polio hutokea zaidi kwa watoto walio na umri chini ya miaka miwili.
Ugonjwa huu unaosababishwa na vijidudu vya virus, huanza kama mafua,
homa, kutapika na maumivu ya misuli kwa mtoto.
Mara nyingine, hizi ndizo dalili zinazoonekana tu. Lakini, wakati mwingine sehemu fulani ya mwili hulegea au kupooza. Mara nyingi hii hutokea kwenye mguu au mkono mmoja. Baada ya muda mguu au mkono uliopooza huwa mwembamba na haukui kwa haraka kama huo mwingine.
Mara nyingine, hizi ndizo dalili zinazoonekana tu. Lakini, wakati mwingine sehemu fulani ya mwili hulegea au kupooza. Mara nyingi hii hutokea kwenye mguu au mkono mmoja. Baada ya muda mguu au mkono uliopooza huwa mwembamba na haukui kwa haraka kama huo mwingine.
FAIDA ZA MWANAUME KUTAHIRIWA
Kutahiriwa ni kitendo cha kuondoa govi au ngozi ya mbele juu inayofunika kichwa cha uume. Hili ni jambo lililokuwa linafanyika kale kwa imani za mira na dini lakini siku hizi hutumika kiafya kwa ajili ya kumkinga mwanaume na magonjwa na maambukizi mbali mbali.
- Inarahisisha kusafisha uume
- Inapunguza uwewzekano wa kupata maambukizi ya njia ya mkojo(U.T.I)
- Inapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya zinaa, malengelenge na UKIMWI
- Inapunguza uwezekano wa kupata kansa ya uume na kumpunguzia mwenza uwezekano wa kupata kansa ya shingo ya kizazi
- Inapunguza hatari ya ngozi kujishikiza kwenye kichwa cha uume moja kwa moja(phimosis)
JITIBU MWENYEWE MAUMIVU YA KIFUA
Maumivu ya kifua usababishwa na matatizo mengi mwili ambapo mengi huwa ni madogo na hayana madhara sana mwilini ila usababisha usumbufu. sana kwa muhusika. Mara nyingi maumivu ya kifua husababishwa na matatizo katika moyo, mapafu, koromeo, mbavu, na kuziba kwa ateri zinazosambaza damu sehemu za mwili na moyo. Endapo unasumbuliwa na maumivu ya kifua kwa muda mrefu au ya papo hapo jaribu kufanya yafuatayo:-
Sunday, 17 August 2014
JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI.
Harufu mbaya ya kinywa husababisha mtu kuwa na hofu au aibu mbele za watu. Hii husababishwa na baadhi ya vyakula, uvutaji wa sigara na tumbaku, midomo kuwa mikavu, kutofanya usafi au maambukizi mbalimbali katika njia ya hewa na chakula.Yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya ili kuondoa au kupunguza harufu mbaya mdomoni:-
- Tibu magonjwa kwanza, hii ni endapo harufu mbaya itakuwa inasababishwa na maambukizi au magonjwa sugu kama meno kuoza, matatizo ya fizi, vidonda mdomoni,magonjwa ya mfumo wa hewa na chakula kwa kutumia dawa utakazoelekezwa hospitali.
- Piga mswaki, asa unapoamka na baada ya kula. Kumbuka kutumia mswaki laini na dawa yenye madini ya fluoride ili kuyapa meno afya bora na kuzuia harufu mbaya. Usisahau pia kusafisha ulimi.
- Sukutua mdomo mara kwa mara, kwa kutumia vinywaji laini au maji safi itakusaidia kuondoa mabaki ya chakula ambayo husababisha harufu mbaya.
- Epuka midomo kuwa mikavu, kwa kupunguza uvutaji wa sigara, tumbaku, unywaji wa pombe. Kunywa maji mengi, kula matunda, kunywa maji mengi, tafuna bigiji na lamba pipi zenye sukari kiasi ili kulainisha midomo yako iwe na unyevu muda mwingi.
- Epuka vyakula vinavyosababisha, kama vile vinavyonata, vyenye sukari nyingi, na kutafuna vitunguu au vitunguu swaumu.
- Badili mswaki walau mara moja kwa miezi mitatu mpaka minne.
- Muone Daktari wa meno na kinywa walau mara moja kwa mwaka kwa uchunguzi na matatizo madogo madogo.
UNAWEZA KUSHUSHA PRESHA KWA KUFANYA HAYA
Mitindo ya maaisha tunayoishi na vyakula tunavyokula hutuweka katika hatari ya kusumbuliwa na shinikizo la damu(Presha). Hii hutokea pale presha inapoongezeka zaidi ya 120/80. Yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya ili kupunguza presha na hivyo kuepuke hatari ya kupata shambulio la moyo, kiharusi na figo kushindwa kufanya kazi.
Saturday, 16 August 2014
FAHAMU KUHUSU MKANDA WA JESHI (HERPES ZOSTER/SHINGLES)
Kwa takribani miongo mitatu sasa, tumeshuhudia ongezeko
kubwa la mlipuko wa ugonjwa wa mkanda wa jeshi linaloendana na ongezeko
la hususani ugonjwa wa UKIMWI. Hali hii imefanya baadhi ya watu kuamini
kuwa, ugonjwa huu ni dalili ya wazi kabisa ya mtu kuwa na VVU, imani
ambayo kwa kiasi kikubwa ina ukweli ndani yake ingawa si kwa wote wanaopatwa nao.Mkanda wa jeshi au shingles au herpes zoster kwa majina ya
kitabibu ni ugonjwa unaosababishwa na virus wa aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga au chickenpox. Ugonjwa huu huathiri ngozi ambapo huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali .
ambayo kwa kiasi kikubwa ina ukweli ndani yake ingawa si kwa wote wanaopatwa nao.Mkanda wa jeshi au shingles au herpes zoster kwa majina ya
kitabibu ni ugonjwa unaosababishwa na virus wa aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga au chickenpox. Ugonjwa huu huathiri ngozi ambapo huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali .
ATHARI ZA KUTUMIA CHUMVI NYINGI KATIKA CHAKULA.
Mara nyingi tumekuwa tukishauriwa kupunguza kiasi cha chumvi kwenye chakula si tu kwa wagonjwa wa kisukari, figo, moyo, ini na presha bali hata kwa mtu mwenye afya nzuri anatakiwa kupunguza kiasi cha chumvi kwa huweza kusababisha matatizo yafuatayo:-
MATUMIZI SAHIHI YA PEDI ILI KUEPUKA MADHARA.
Wanawake wanashauriwa kufanya yafuatayo ili kuhakikisha usalama wa afya zao watumiapo pedi :
1. Kunawa mikono vizuri kwa sabuni kabla ya kugusa pedi ambayo unatarajia kuivaa na baada ya kuvaa kunawa tena mikono vizuri.
2. Kutohifadhi pedi bafuni au chuoni au sehemu yote yenye unyevunyevu na isiyo na mwanga wa kutosha ili kutotengeneza mazingira ya kukua kwa vimelea vya magonjwa ndani ya pedi.
3. Kuangalia kwa makini muda wa matumizi ya pedi kabla ya kununua au baada ya kutunza pedi kwa muda muda mrefu ili kuepuka kutumia pedi zilizopita muda wake wa matumizi.
4. Kuepuka kununua pedi zinazouzwa kiholela na zisizothibitishwa na TBS na mamlaka nyingine zenye dhamana ya kuangalia ubora wa pedi hizo. Mwanamke anatakiwa kuangalia nembo ya uthibitisho wa mamlaka hizo na kujiridhisha kuhusiana na usalama wa pedi hizo kabla hajanunua.
5. Kubadilisha pedi kila baada ya masaa mawili, kama tunavyojua damu ni moja wapo ya chakula kizuri sana kwa vimelea vya magonjwa kama bacteria ,unyevunyevu unaosababishwa na kuvaa pedi kwa muda mrefu pia unapelekea ustawi wa bacteria hao na joto ambalo lipo katika maumbile ya ndani ya mwanamke vikiungana kwa pamoja vinatengeneza mazingira mazuri ya ukuaji wa bacteria , hivyo wanawake wanashauriwa kutovaa pedi hizo kwa muda usiozidi masaa mawili ili kuepuka mazingira hayo.
6. Kuchagua aina sahihi inayokutosha ina kuepuka pedi zinazobana sana kupita kiwango sababu zinaweza pia kukufanya usiwe huru na kutengeneza joto la ziada na michubuko katika maumbile ya mwanamke,hivyo mwanadada unashauriwa kutumia pedi itakayokukaa vizuri(isilegee sana wala kuachia sana)
7. Kwa wadada wanaotumia vitambaa badala ya pedi ni muhimu pia kuzingatia kanuni za kiafya na usafi kabla na baada ya kutumia vitambaa hivyo kama vile kuchagua kitambaa angavu ,kukiloweka na kukifua vizuri, kuanika kwenye sehemu yenye mwanga wa jua wa kutosha na upepo wa kutosha pasipo na unyevunyevu ,kupiga pasi kabla ujakihifadhi na kabla ya kutumia ili kuuwa vimelea vya magonjwa
MAMBO YANAYOSABABISHA MWANAMKE KUKOSA MTOTO
- Uterine Septum(Mfuko wa uzazi kutengana)
- Blockage(kuziba kwa mirija ya uzazi)
- Polycystic Ovaries( Vimbe nyingi katika ovari)
- Polyps(Tishu za ukuta wa mji wa mimba kujitokeza ndani ya mji wa mimba)
- Infections(Maambukizi)
- Fibroids (Uvimbe)
- Endometriosis(Tishu za mfuko wa uzazi kujishikiza nje ya mfuko wa uzazi)
- Scar tissue(Makovu katika njia ya uzazi)
NJIA ZA KUKUSAIDIA KUZUIA MIMBA
Kama wewe na mpenzi wako hawataki kuwa na mtoto kwa
wakati huu, unaweza kuuliza "jinsi ya kuzuia mimba?". Bahati nzuri, kuna
bidhaa nyingi tofauti ambayo inaweza kusaidia kuzuia mimba. Aina ya
uzazi ambayo ni ya uhakika kwa ajili ya kuzuia mimba ni kuzaliwa
kudhibiti dawa, sindano, implantat, IUDs, na sterilization. Ya wanawake
100 ambao kila kutumia moja ya aina hizi za uzazi wa majira kwa mwaka,
juu ya 1 hadi 5 wanawake mimba.
Friday, 15 August 2014
BANGI ILIVYOOKOA MAISHA YA MTOTO MDOGO
Mwanamke mmoja Rachael Garner kutoka Florida anaamini bangi ndio iliokoa maisha ya mwanae mwenye umri wa miezi 19 baada ya madaktari kushindwa kumtibu matatizo ya kupooza ubongo na ubongo kujaa maji yaliyokuwa yakimsababishia ugonjwa wa kifafa.
MWANAMKE AJINYONGA KATIKA TAMASHA LA MUZIKI
Lisa Williamson, kutoka Bromyard ni mwanamke aliyejinyonnga katika Hampshire lililofanyika siku ya jumamosi katika mji wa Winchester na kushirikisha watu zaidi ya 38,000. Hili ni tukio la pili kutokea katika tamasha hili kwani mwaka jana pia kijana mmoja aitwaye Ellie Rowe mwenye umri wa miaka 18 alijiua kwa ktumia dawa za ketamine.
UNENE UNAWEZA KUKUSABABISHIA SARATANI ZIFUATAZO
Unene kupita kiasi ni hatari sana na unaweza kukuweka katika hatari ya kupata saratani zifuatazo kwa kila kilo 13-16 zinazoongezeka katika mwili wako
- Saratani ya mfuko wa uzazi
- Saratani ya mlango wa kizazi
- Saratani ya nyongo
- Saratani ya figo na kibofu
- Saratani ya tezi ya thairoidi
- Kansa ya damu
- Kansa ya utumbo mkubwa
- Saratani ya matiti.
Thursday, 14 August 2014
UONAPO DALILI HIZI USIPUUZE ZINAWEZA KUPELEKEA KIFO.
Mara nyingi mwili wa binadamu hutoa dalili na ishara kuonyensha kuwa kuna kasoro inayoendelea kutokana na magonjwa au tatizo lolote la kiafya ambapo wengi wetu hatuchukulii kiundani ishara hizi na kuuacha mwili ufanye kazi na kukabiliana na kasoro wenyewe. Kuna baadhi ya dalili huwa ni hatari sana hivyo hupaswi kudharau wala kupuuza bila kufika kituo cha afya au hospitali.
Wednesday, 13 August 2014
NAMNA KUJITIBU MAFUA
Mafua ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya mafua na uambatana na homa kali, kutojiskia vizuri, maumivu ya kichwa na dalili nyingi ambazo humfanya mtu kukosa nguvu. yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya nyumbani ili kujitibu ugonjwa huu ila usikose kwenda hosipitali kama yote yatashindikana au mafua yanaambatana na dalili nyingine kama kikohozi au kutokupona kwa muda mrefu.
FANYA YAFUATAYO KUZUIA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA KIPINDI CHA UJAUZITO
- Kula milo mingi midogo mara kwa mara badala ya kula milo mikuu mitatu kwa siku. Hii itasaidia kwasababu wakati mwingine tatizo hili linasababishwa na kutokuwa na sukari ya kutosha kwenye damu(low blood pressure). Sukari hii ndio chanzo cha nguvu mwilini. Ukila mara kwa mara chakula kitapokelewa mwilini na kutengenezwa sukari na mwili kuwa na nguvu ya kutosha.
- Kunywa vinywaji nusu saa kabla au baada ya chakula. Usinywe vinywaji na kula chakula kwa wakati mmoja.
MAZOEZI 7 YANAYOFAA KWA MAMA MJAMZITO
Haya ni mazoezi 7 muhimu sana kwa mama mjamzito. Usikose kutembelea blog hii kila siku kwa maelekezo jinsi ya kufanya mazoezi haya.
DALILI NA MATIBABU YA TETE KUWANGA
Tete kuwanga au Chicken pox ni ugonjwa ambao uambukiza nakusababishwa
na virusi vinavyojulikana kama Varicella zoster. Maambukizi ya
tete kuwanga huonekana sana kwa watoto wadogo ingawa hata watu wakubwa
pia hupata maambukizi ya ugonjwa huu. Tete kuwanga hupatikana duniani
kote asa katika nchi zenye kupata majira ya baridi. Tete
kuwanga huambukizwa kupitia njia ya hewa au kugusana mwili
na mgonjwa wa tete kuwanga(kupitia majimaji yanayotoka kwenye vipele vya mgonjwa au anapokohoa.
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA.
Wizara ya afya na ustawi wa jamii imetoa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola na kuwataka wananchi kujikinga na kutokuwa na hofu endapo ugonjwa huu utaingia hapa nchini. Kujua dalili, njia za kujikinga soma zaidi kutoka tovuti ya wizara ya afya http://www.moh.go.tz/images/newsroom/Press_Release_2.pdf
Tuesday, 12 August 2014
HOMA YA MAPAFU KWA WATOTO WADOGO (PNEUMONIA)
Homa ya mapafu au Pneumonia ni ugonjwa unaosababishwa na wadudu, virusi, fangasi na bakteria kama Escherichia, streptococci, RSV, Streptococcus pneumoniae, Mycoplasma pneumoniae,kifaduro, na virusi vya mafua ambao ushambulia njia ya hewa na mapafu asa kwa watoto wadogo chini ya miaka miwili.
Dalili za ugonjwa wa homa ya mapafu
Dalili za kawaida za homa ya mapafu ambazo huwapata karibu watoto wote
wanaoathirika na ugonjwa huu ni pamoja na:TATIZO LA KUWASHWA LIPS NA TIBA YAKE
Hili ni tatizo ambalo mtu uhisi kuwashwa na kuwa na hamu ya kujikuna ngozi au kuvimba sehemu za mdomo(Lips). Hii husababishwa na vipodozi, lipsticks, vyakula, mazingira na magonjwa mbalimbali asa malengelenge, magonjwa ya ngozi, chango, saratani, kuchafuka kwa damu, ukurutu, matatizo katika nyongo, ukosefu wa vitamini nk.
MASKIO YALIYOUNDWA KUTOKA UBAVUNI
Kijana huyo wa miaka tisa Kieran Sorkin alizaliwa bila masikio na madaktari wamekuwa wakifanya majaribio ya mbinu mpya ya matibabu katika hospitali ya Great Ormond Street iliyoko jijini London..
Takwimu nchini Uingereza zinaonesha kuwa takriban watoto 100 huzaliwa bila kiungo hicho muhimu nchini Uingereza .
ZMAPP DAWA YA KUTIBU EBOLA
Jopo la wataalam wa shirika la afya duniani WHO
limeamua kwamba watu wanaweza kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa katika
mwili wa binaadamu kutibu ugonjwa wa ebola,iwapo maagizo fulani
yataheshimiwa ikiwemo ruhusa ya mgonjwa.
Sunday, 10 August 2014
CARTOON: IKER CASILLAS AENDELEA KUWA BOSS MADRID
ARSENAL KUTUMIA PESA NYINGI KULIKO MANCHESTER CITY
SOMA ZAIDI http://duniaadaa.blogspot.com/2014/08/usajili-wa-arsenal-kugharimu-pesa.html
ARSENAL YATOA ONYA KWA MABINGWA WA EPL
Ikiwakosa wachezaji wake tegemezi Per Mertesacker, Mesut Ozil na Lukas Podolski timu ya Arsenal imefanikiwa kutoa onyo kali kwa vijna waPellegrini baada ya kuwachakaza bao 3-0 mabao yaliyofungwa na Santi Cazorla, Aaron Ramsey and Olivier Giroud na kuwawezesha kushinda ngao ya jamii. Pamoja na kuwakosa nyota wake saba wa kikosi cha kwanza Manchester City walizidiwa karibu kila idara huku Arsenal wakitawla mchezo kwa muda wote na kufanikiwa kupata ushindi huo.
Saturday, 9 August 2014
TATIZO LA UKE KUWA MKAVU NA MATIBABU YAKE
Tatizo la kuwa na uke mkavu hutokana na kupungua kwa hormoni aina ya estrojeni katika mwili wa mwanamke ambayo husababisha kudhoofika na kusinyaa kwa misuli ya uke kukosa vilanisho. Hii utokea mara nyingi kwa wanawake wasioskia hamu ya tendo la ndoa, waliojifungua, wanaonyonyesha, wazee na ambao wako katika hedhi. Hii huweza kusababisha maumivu makali kipindi cha tendo na kukuweka katika hatari ya kupata maambukizi ya zinaa na UTI
KUPUNGUZA UZITO UKUSAIDIA KUPAMBANA NA MAGONJWA HAYA SUGU.
Uzito uliozidi kiasi unakuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa mengi
sugu kwa mfano, kisukari, msukumo mkubwa wa damu, magonjwa ya moyo,
figo, saratani na mengineyo. Magonjwa haya yanaleta kifo mapema na
matatizo mengine mengi…. Jizoeshe taratibu za kula ambazo zitakusaidia
kupunguza uzito au kuzuia ongezeko kubwa la uzito..Badili mtindo wa
kula, yafuatayo yanaweza kukusaidi:
Friday, 8 August 2014
TATIZO LA KUWASHWA KATIKA NJIA YA AJA KUBWA
Kuwashwa sehemu ya haja kubwa au katika ngozi inayozunguka sehemu hizo ni tatizo ambalo huwapata watu wengi wengi mara kwa mara na husababishwa na maambukizi, uchafu, baadhi ya vyakula na au kuumia ambavyo husababisha mtu kujikuna sana.
WHO:'Ebola ni janga la kimataifa
Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuenea kwa
ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa afrika kama janga la kimataifa
linalohitaji kushughulikiwa kwa dharura.
Subscribe to:
Posts (Atom)