Sunday 2 November 2014

DALILI ZA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI:

Mwili wa binadamu unaitaji sana sukari kwa ajili ya matumizi ya kila siku na unapokosa au kupungukiwa na sukari sehemu ya kwanza kuhadhirika huwa ni ubongo. Zifuatazo ni dalili zitakazokuwezesha kutambua kama una upungufu wa sukari mwilini na kujitibu mapema ili kuepuka madhara:-
1. Uchovu na mwili kukosa nguvu
2. Kutetemeka na kuskia mapigo ya moyo yanakwenda haraka.
3. Ngozi kusinyaa au kubadilika rangi.
4. Kutokwa na jasho sana.
5. Hasira na kuchanganyikiwa.
6. Maumivu makali ya kichwa.
Dalili ambazo ni hatari na hutokea baadae ni pamoja na maumivu makali ya kichwa, kushindwa kutembea vizuri, udhaifu au kutetemeka ulimi na mdomo na kupoteza fahamu.

No comments:

Post a Comment

.