Wanasayansi wanasema kuwa
kufanya kazi katika muda usio wa
kawaida kikazi au katika mazingira
yaliyo ya upweke kunaweza
kuzeesha ubongo na kufanya
uwezo wa utendaji kuwa duni.
Utafiti huo umeeleza katika jarida la
Occupational and Environmental
Medicine kuwa iwapo kazi za
kupokezana, mfano nyakati za usiku
zitafanywa kwa takriban miaka kumi
mfululizo zitazeesha ubongo kabla ya
wakati wake.
Wanasayansi wanasema ahueni
imeonekana kwa watu baada ya
kuacha kufanya kazi hizo lakini
ilichukua miaka mitano kurejea
kwenye hali ya kawaida.
Utafiti huu unaelezwa kuwa muhimu,
kwa kuwa waathiriwa wengi kutokana
na tatizo hilo wamekuwa wakilala
usingizi wa mang'amung'amu.
Moja ya madhara yatokanayo na
kufanya kazi usiku ni kuongezeka
uzito kupita kiasi
Wataalam hawa wameiambia BBC
kuwa miili na akili zimejengwa kwa
kufanya kazi mchana na kulala
nyakati za usiku.
Athari mbaya ambazo zinaelezwa
kutokana na mtindo huo wa ufanyaji
kazi ni madhara ya Saratani na uzito
mkubwa.
Timu ya wanasayansi kutoka chuo
cha Swansea na Toulouse
wameonesha kuwa kuna madhara ya
kiakili pia.
Wednesday, 5 November 2014
MADHARA YA KUFANYA KAZI USIKU.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment