Saturday 22 November 2014

KAMA UNASUMBULIWA NA HARUFU MBAYA YA KWAPA.

Harufu ya kwapa haisababishwi na kutokwa na jasho bali bakiteria wanaovutiwa na jasho au unyevu chini ya kwapa. Hii umkosesha mtu ujasiri na kujiamini, au kuwa kero mbele za watu. Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo



  • Paka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa  safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya
  • Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya
  • Oga kila siku na safisha nguo kwa maji safi itasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya
  • Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.
  • Osha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa(medicated soaps)
  • Punguza kula chakula chenye viungo vingi asa vitunguu, vitunguu swaumu na pilipili
  • Kumbuka kutumia pafyume na Spray zitasaidia kuondoa harufu mbaya kwa muda na sio kutibu tatizo moja kwa moja.
  • Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili.
  • Jitahidi kunyoa nywele za sehemu hii mara kwa mara.
  • Epuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.
KAMA UNASUMBULIWA NA TATIZO LOLOTE LA KIAFYA WASILIANA NASI

No comments:

Post a Comment

.