Sunday 2 November 2014

SABABU NA DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.

Ugonjwa huu husababishwa na
virusi vinavyoitwa Human papilloma,
ambapo mtu anaweza kupatwa na
virusi hawa wakati wa kujamiana na
mtu mwenye maambukizi. Human
Papillomavirus aina ya 16 na 18
husababisha kansa ya aina hii kwa
asilimia 75 duniani kote huku aina ya
31 na 35 zikisababisha maambukizi
kwa asilimia 10. Watu walio katika
hatari ya maambukizi ya ugonjwa
huu ni kwa ujumla wanawake wote
lakini zaidi wale wasiokwenda
kufanyiwa uchunguzi wa kila mwaka
kuhusiana na ugonjwa huu
unaojulikana kitaalamu kama pap
smear, wanawake walioathirika na
virusi vya human papillomavirus
HPV au genital warts, wanaovuta
sigara, wenye ukimwi na wasiokula
vyakula bora hasa wasiozingatia
mboga na matunda katika lishe zao.
Kutokana na uchunguzi huo, timu ya
wataalamu wa ugonjwa huo
imeeleza sababu zinazochangia
kupata saratani ya shingo ya kizazi
na kubainisha dalili ambazo
huonekana kwa mtu ambaye
anasumbuliwa na ugonjwa huo.
Kimsingi mabadiliko ya awali ya
saratani hii hayatoi dalili yoyote ya
moja kwa moja hadi mwanamke
afanyiwe uchunguzi au vipimo
vingine vya ugonjwa huo. Dalili
zinazoonesha kuwepo kwa saratani
ya shingo ya kizazi ni pamoja na
kutokwa na damu ambayo si ya
hedhi, kutokwa na uchafu, majimaji
au usaha sehemu za siri. Hata hivyo
dalili nyingine ni pamoja na kuhisi
maumivu makali wakati wa
kujamiiana na kusababisha kutokwa
na damu baada ya tendo hilo
ambapo pia ni pamoja na maumivu
ya tumbo chini ya kitovu sambamba
na maumivu ya kiuno.
Kufanyiwa uchunguzi wa pap smear
ili kubaini ugonjwa huu kuna nafasi
kubwa katika kuzuia watu kupatwa
na saratani ya shingo ya kizazi.
Uchunguzi wa awali wa saratani ya
shingo ya kizazi unatakiwa kufanyiwa
wanawake walio katika mahusiano
ya ndoa na pia wanatakiwa kupima
mara kwa mara hadi wanapofikia
umri wa miaka 69. Mwanzoni
uchunguzi huu unatakiwa ufanyike
mara kwa mara kwa muda wa miaka
mitatu mfululizo. Ikitokea katika
miaka mitatu mfululizo uchunguzi
huo haujatoa dalili zozote za
kuwepo saratani basi mwanamke
anaweza kuendelea kufanyiwa
uchunguzi mara moja kila baada ya
miaka miwili na mitatu hadi pale
atakapofikisha umri wa miaka 69.

No comments:

Post a Comment

.