Monday 10 November 2014

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (Ovarian cyst)

Uvimbe kwenye mayai ya
mwanamke (ovary) hutokana na
mkusanyiko wa majimaji
yanayozungukwa na kuta
nyembamba ndani ya mayai ya
mwanamke. Uvimbe huu ambao
hupatikana ndani ya mayai ya
mwanamke ndio unaojulikana kama
ovarian cyst. Uvimbe huu hutokea
kwa wanawake wa umri wowote ule


na mara nyingi huonekana kwa
wanawake waliofikia kikomo cha
umri wa kupata ujauzito. Lakini
kwanza hebu tuelezee juu ya mayai
ya mwanamke. Kwa kawaida
mwanamke anakuwa na mayai
mawili katika mwili wake. Yai moja
upande wa kulia na yai jingine
upande wa kushoto kwake. Mayai
haya hupatikana pembezoni mwa
mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya
ya mwanamke huanza kuzalisha
mayai ya uzazi yanayojulikana kama
ovum na mayai hayo ya uzazi
hukuwa ndani ya mayai ya
mwanamke (ovary) kwa kuchochewa
na baadhi ya homoni. Katikati ya
mwezi, siku ya kumi na nne, masaa
24-36 baada ya kiwango cha
kichocheo aina ya Luteinizing
Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi
hutolewa katika kila ovari na hii ndio
hujulikana kama ovulation au kufikia
kilele upevukaji mayai. Mayai haya ya
uzazi huishi kwa masaa machache
hadi masaa 24 ikiwa
hayatorutubishwa na mbegu kutoka
kwa mwanamume. Mabaki ya mfuko
wa mayai ya uzazi yanayojulikana
kama follicle ndani ya ovari, hugeuka
na kuwa corpus luteum ambao
huhusika na utoaji wa kichocheo au
homoni aina ya progesterone kwa
wingi. Homoni hii ya progesterone
ndio inayosababisha mfuko wa
uzazi kujiandaa kwa kujikita yai
(implantation) lililorutubishwa kwa
mbegu ya kiume ndani ya mfuko wa
uzazi kwa kuongeza unene kwenye
kuta zake. Yai hili husafiri hadi
kwenye mfuko wa uzazi ambako
hukua na kuwa mtoto. Kama
upachikwaji wa yai liliorutubishwa
hautafanyika, basi ndani ya wiki
mbili, corpus luteum huanza
kusinyaa na kupotea na kusababisha
kushuka kwa kiwango cha homoni
aina ya progesterone na estrogen.
Kushuka kwa viwango vya vichocheo
hivi ndio husababisha mfuko wa
uzazi kuanza kutoa mabaki ya kuta
zake pamoja na yai la uzazi na hii
ndiyo pale mwanamke anapotoka
damu ukeni inayojulikana kama
hedhi. Unaweza ukajiuliza, ni kwa
nini nimeanza na maelezo haya,
lakini jibu ni kutaka kuonyesha
umuhimu wa mayai ya uzazi kwa
mwanamke pamoja na kazi yake.
&&&&
Kuna aina ngapi za uvimbe kwenye
mayai ya mwanamke?
Kuna aina nyingi za uvimbe kwenye
mayai ya mwanamke lakini aina hizi
saba ndio huonekana sana kwa
wanawake wengi ambazo ni kama
ifuatavyo:
I. Follicular cyst ni uvimbe ambao
hutokea wakati ovulation isipotokea
au baada ya corpus luteum kuanza
kusinyaa na kupotea yenyewe baada
ya kutopachikwa kwa yai kwenye
kuta za mfuko wa kizazi. Uvimbe huu
unakuwa na wastani wa inchi 2.3
kwa upana. Upasukaji wa uvimbe
huu husababisha maumivu makali
sana katikati ya mzunguko wa hedhi
yaani siku ya ovulation. Maumivu
haya huonekana kwa robo ya
wanawake wenye aina hii ya uvimbe.
Kwa kawaida, uvimbe huu hauna
dalili zozote na hupotea wenyewe
baada ya miezi kadhaa.
II.Corpus Luteum cyst- ambao ni
uvimbe unaotokana na
kutopachikwa kwa yai la uzazi
lililorutubishwa na mbegu ya kiume
kwenye mfuko wa kizazi. Kwa
kawaida corpus luteum husinyaa na
kupotea yenyewe, au wakati
mwengine inaweza ikajaa maji na
hivyo kusababisha uvimbe wa aina
hii. Uvimbe huu huonekana kwenye
upande mmoja (kushoto au kulia)
wa mwanamke na hauna dalili
zozote zile.
III. Hemorrhagic cyst- Uvimbe huu
hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa
damu ndani ya uvimbe wa aina
yoyote ule ambao
umeshajitengeneza tayari.
Huambatana na maumivu makali
kwenye upande mmoja wa ubavu
wa mwanamke (kushoto au kulia).
IV. Dermoid cyst- Uvimbe huu
ambao sio saratani na pia
hujulikana kama mature cystic
teratoma, huathiri wanawake
wadogo walio katika umri wa
kushika mimba na huweza kukua na
kufikia inchi 6 kwa upana na ndani
yake huweza kuwa na
mchanganyiko wa nywele, mfupa,
mafuta na cartilage. Uvimbe wa aina
hii huweza kuwa mkubwa zaidi au
kujizungusha na hivyo kuathiri
usambazaji wa damu kwenda
kwenye uvimbe huu na hivyo
kusababisha maumivu makali sana
maeneo ya tumboni.
V. Polycysitic appearing cyst- Uvimbe
wa aina hii unakuwa ni mkubwa
sana na huwa umezungukwa na
vijivimbe vyengine vidogo vidogo na
huonekana hata kwa wanawake
wenye afya njema au wale wenye
matatizo ya homoni.
VI. Cystedenoma-Ni aina ya uvimbe
unaotokana kwenye tishu za ovary
na hujazwa na majimaji yenye
kuvutika. Uvimbe wa aina hii huweza
kuwa mkubwa sana hata kufikia
inchi 12 au zaidi kwa upana.
VII. Endometriomas /Endometrial
Cysts- Husababishwa na uwepo wa
aina mojawapo ya kuta za mfuko wa
kizazi unaojulikana kama
endometrium kwenye mayai ya
mwanamke. Huathiri wanawake
waliofikia kikomo cha umri wa
kupata ujauzito na huambatana na
maumivu sugu ya nyonga wakati wa
hedhi. Uvimbe huu unakuwa na
damu ya rangi nyekundu
inayoelekea kuwa kahawia na
ukubwa wake ni kuanzia inchi 0.75
hadi 0.8.
&&&
Nini husababisha tatizo hili la
uvimbe kwenye mayai ya
mwanamke?
Vihatarishi vya tatizo la uvimbe
kwenye mayai ya mwanamke ni;
kwanza kabisa historia ya awali ya
ovarian cyst. Kwa maana kuwa,
wanawake ambao wazazi wao au
watu wao wa karibu wamekuwa
wakisumbuliwa na ugonjwa huo
kuna uwezekano mkubwa nao pia
wakapatwa na tatizo hilo. Sababu
nyingine inayoweza kusababisha
uvimbe katika mayai ya mwanamke
ni kuwa na mzunguko wa hedhi
usiokuwa na mpangilio maalum au
kama tunavyouita kwa kimombo,
irregular menstruation cycle.
Kihatarishi kingine ni kuwa na
mafuta mengi kwenye sehemu ya
juu ya mwili na hii ni kwa wale
wanawake wanene. Ugumba na
kuvunja ungo au kubaleghe
mapema ni sababu nyingine
ambapo mtoto wa kike
anapobaleghe akiwa na miaka 11 au
chini ya hapo huweza kupatwa na
uvimbe katika mayai yake. Vilevile
kukosekana uwiano sawa wa
vichocheo au homoni mwilini au
ugonjwa wa hypothyroidism na pia
dawa ya kutibu saratani ya matiti ya
Tamoxifen husababisha tatizo hilo.
Dalili na viashiria vya Ovariancyst.
a)Maumivu makali, ambayo hayana
mwanzo maalum na yanayochoma,
ambapo maumivu hayo yanaweza
yakawa yanakuja na kupotea au
yakawepo moja kwa moja. Pia mtu
anaweza kupata usumbufu na
kutojisikia vizuri kwenye maeneo ya
chini ya kitovu, kwenye nyonga, uke,
kwenye mapaja na mgongoni
upande wa kwa chini. b) Kuhisi
tumbo kuwa zito, kujaa au kuvimba.
c) Maumivu kwenye matiti na hedhi
isiyokuwa na mpangilio maalum.
d) Maumivu ya muda mrefu kwenye
nyonga wakati wa hedhi na ambayo
huweza kuhisiwa sehemu ya chini
mgongoni. Maumivu haya yanaweza
kuanza muda mfupi tu baada ya
kuanza hedhi, wakati wa hedhi au
mwisho wa hedhi.
e) Maumivu ya nyonga baada ya
kufanya kazi ngumu, mazoezi au
baada ya kujamiiana. Kuhisi
kichefuchefu, kutapika na kutokwa
na matone ya damu ukeni. Dalili
nyingine ni ugumba na kuhisi
uchovu, mabadiliko ya haja ndogo
yaani kukojoa mara kwa mara,
kujikojolea au kushindwa kutoa
mkojo wote kutoka kwenye kibofu
cha mkojo wakati wa kupata haja
ndogo.
Vilevile mabadiliko ya haja kubwa
ambayo ni kupata haja kubwa kwa
shida sana kutokana na presha
kwenye maeneo ya nyonga.
n) Nywele kukua kwa kasi na
kuongezeka kuota kwa nywele
kwenye uso au sehemu nyingine za
mwili. Dalili nyingine za uvimbe
katika mayai ya mwanamke ni
kuumwa kichwa, kuongezeka uzito,
maumivu ya kwenye mbavu,
kutokewa na uvimbe chini ya ngozi
na kuvimba mara kwa mara.
Vipimo vya uchunguzi:- Kwanza
kabisa ni mgonjwa kufanyiwa
Endovaginal Ultrasound ambayo
hufanywa kwa kuingiza mpira
maalum kupitia ukeni na kuangalia
mfuko wa uzazi na mayai ya
mwanamke. Kwa kutumia kipimo
hiki, ni rahisi kwa daktari kugundua
kama uvimbe kwenye mayai ni wa
aina gani na kujua kama ni maji tu
(fluid filled sac), au ni maji pamoja
na mchanganyiko wa vitu vigumu
kwa mana ya complex, au ni vitu
vigumu pekee ambapo huitwa
completely solid. Kipimo kingine
kinachochukuliwa kuchunguza
ugonjwa huu ni Abdominal Pelvic
Ultrasound ambayo ni Ultrasound ya
kawaida. Husaidia kujua ni aina gani
ya uvimbe uliopo kwenye mayai ya
mwanamke.
Wapenzi wasikilizaji tunaishia hapa
kwa leo lakini bado hatujamaliza
kuelezea vipimo vyote
anavyochukuliwa mwanamke
mwenye uvimbe katika mayai. 

Kutoka: ISR

No comments:

Post a Comment

.