Monday, 10 November 2014

SHERIA KALI KWA WANAOVUTA SIGARA HADHARANI.

Suala la watu wengi kutopendezwa na kitendo cha baadhi ya watu kuvuta sigara hadharani ama ndani ya vyombo vya usafiri limekuwa likizungumziwa sehemu mbalimbali na ikafika wakati hata Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliwahi kujadili kuhusu kutengenezwa sheria itakayopiga marufuku.
Leo kuna taarifa mpya, unajua bunge la Uingereza limewasilisha mapendekezo ya sheria itakayopiga marufuku uvutaji wa sigara hadharani?

Mwezi February 2015, tutarajie mabadiliko makubwa Uingereza ambapo inatarajiwa sheria ya familia na watoto kupitishwa iwapo Bunge la Uingereza litaidhinisha Sheria hiyo ambayo inapiga marufuku uvutaji wa sigara ndani ya vyombo vya usafiri wa abiria kwa ajili ya kuwalinda watoto.
Katibu Mkuu wa Wizara ya afya Uingereza, Jeremy Hunt anatarajiwa kutangaza kuhusu mabadiliko yatakayotokana na Sheria hiyo mwezi ujao, japo baadhi ya wachambuzi hawaoni kama kupitishwa kwa sheria hiyo kutasaidia kutatua tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment

.