Friday 14 November 2014

KWA WAOVAA MIWANI SOMA HAYA NA UYAZINGATIE ILI KUEPUKA UPOFU WA KUDUMU.

Watu zaidi ya million huvaa miwani ambayo huwawezesha kuona vizuri au hutumika kama urembo. Hata hivyo miwani hii huweza kusababisha maambukizi na upofu wa macho endapo haitasafishwa mara kwa mara na kutunzwa vyema kwani bakteria, fangasi na vijidudu vingine hatari huweza kuingia katika macho na kusababisha upofu wa kudumu.

Njia sahihi za kutunza miwani na kujikinga na madhara haya ni pamoja na kufanya yafuatayo:-
Nawa mikono kwa maji safi na sabuni kisha ikaushe kabla ya kugusa au kufuta kioo cha miwani yako.
Sugua na isafishe kwa kitambaa safi na dawa pale unapoivua.
Tumia miwani pekee uliyoelekezwa na wataalamu wa macho.
Baadhi ya miwani huuzwa pamoja na dawa kwa ajili ya kusafishia na usitumie dawa uliyotumia kwa miwani ya aina tofauti kusafisha.
Usitumie mate au maji kusafisha miwani na pia usiifadhi katika maji au unyevunyevu.
Usilale, kuoga au kuogelea na miwani isipokuwa kama umeelekezwa vinginevyo na wataalamu wa macho.
Waone wataalamu wa macho walahu mara moja kwa mwaka kwa ushauri kuhusu kubadili miwani.
Nenda hosipitali mapema unapohisi maumivu, kuvimba au kutoona vizuri.
BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA WAELIMISHE MARAFIKI. 


No comments:

Post a Comment

.