Thursday 13 November 2014

KUWA MAKINI NA MAZINGIRA YANAYOWEZA KUATHIRI AFYA YAKO.

Mazingira ni jambo lingine
linaloathiri afya. Iwapo maji
tunayokunjwa na kutumia ni safi na
salama, iwapo hewa tunayovuta si
chafu, maeneo tunayofanyia kazi ni
salama na pia nyumba tunazoishi,
basi afya zetu huwa salama zaidi
ikilinganishwa na watu wanaoishi
kwenye maeneo yasiyo na maji safi
na salama au kuvuta hewa chafu na
kufanya kazi kwenye mazingira ya
hatari. Uchunguzi uliofanywa na
chuo kikuu cha Zuyd nchini
Uholanzi umeonesha kwamba,
kuvuta hewa iliyochafuliwa kwa gesi
za magari kwa lisaa limoja
kunatosha kumpatia mtu mfadhaiko
wa kifikra au stress katika ubongo
wake. Utafiti mwingine uliofanywa
na chuo kikuu cha India cha Purdue
umebainisha kuwa, sumu kali
inayotokana na sumu ya risasi,
inayoweza kuiingia mwilini mwa
binadamu kutokana na kula vitu
vilivyoingiwa na sumu hiyo, nchini
Marekani huathiri maelfu ya watoto
kuliko kiwango dhaifu cha sumu
hiyo kinachoweza kuwepo katika
vifaa vya kuchezea na mapambo
yanavyosafirishwa.
Afya ya binadamu pia huweza
kuathiriwa na watu
wanaomzunguka. Iwapo una familia
unayoiangalia au marafiki katika
jamii yako, basi una nafasi kubwa ya
kuimarisha afya yako kuliko mtu
ambaye anaishi pekee au hana
familia na marafiki. Uchunguzi
uliofanywa na chuo kikuu cha
Washington nchini Marekani
umegundua kuwa, ushirikiano wa
kifamilia ni jambo zuri kwa mtu na
hupunguza kesi za atu kujiua, hasa
wale wanaopatwa na matatizo ya
mfadhaiko wa kifikra au
wanapokuwa na fikra ya kutaka
kujiua. Vilevile tamaduni, mila na
desturi za jamii na jinsi watu
wanavyozithamini itikadi hizo, zina
mafasi kubwa katika afya zao ingawa
matokeo yake huweza kuwa mazuri
au mabaya. Kwa mfano mazoea na
mila ya kuwakeketa au kuwatahiri
watoto wa kike na wanawake ina
madhara makubwa kama vile
kuongeza kiwango cha maambukizo
ya magonjwa na hata matatizo ya
kiakili miongoni mwa wasichama na
wanawake wanaofanyiwa jambo
hilo. Utafiti uliochapishwa katika
Jarida la Afya ya Jamii na Elimu ya
Magonjwa ya Mlipuko umebainisha
kuwa, wakati vijana wanapovaa
mavazi kwa mujibu wa mila na
tamaduni za makundi au makabila
yao, suala hilo huweza
kuwapunguzia uwezekano wa
kupatwa na matatizo ya kiakili
baadaye maishani.

No comments:

Post a Comment

.