Sunday 9 November 2014

VYANZO VYA UGONJWA WA U.T.I KWA WANAWAKE WENGI.

Vyanzo vinavyosababisha ugonjwa wa UTI ni matumizi ya maji  machafu wakati wa kujisafisha au kuoga ambayo huweza kuweka bakteria kwa urahisi na mwanamke kupata UTI.
Uchafu wa vyoo ni sababu nyingine asa matumizi ya vyoo ambavyo ni vichafu. Chooni kuna bakteria wengi ambao wanaweza kusababisha UTI.
Pia kufanya ngono mara kwa mara ni tatizo kubwa ambalo ndilo linafanya wanawake wengi kupata UTI siku hizi, kwani wakati wa ngono msuguano huwa mkubwa ambao hufanya bakteria kutoka kupitia majimaji ya ukeni na kuingia katika njia ya mkojo.
“Mwanamke ambaye anafanya ngono mara kwa mara yuko kwenye hatari ya kupata UTI kuliko yule ambaye hafanyi ngono mara kwa mara.
 Pia matumizi ya nguo za ndani za mitumba bila kufua husababisha kwa urahisi mwanamke kupata UTI. Hata hivyo kemikali zinawaathiri wanawake wengi siku hizi,  kutumia sana kemikali hasa kwenye vipodozi na sabuni ambavyo kemikali hizi kwa kuwa ni sumu huenda hadi kwenye kibofu na kuchubua kibofu na hapo ndipo tatizo hilo huanza.”
Wataalamu wamesisitiza kwamba wengi wamekuwa na tabia ya kubana mkojo kwa muda mrefu, lakini matokeo ya tabia hii ni kupata UTI. BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA WASILIANA NASI KWA TIBA NA USHAURI

No comments:

Post a Comment

.