Monday 3 November 2014

UGONJWA MWINGINE TISHIO BAADA YA EBOLA.

Ugonjwa wa homa ya Lassa Afrika
Magharibi unaelezwa kusahaulika
kutokana na mlipuko wa ugonjwa
wa Ebola na Wahudumu wa afya
wamesema huenda wakakosa
rasilimali kukabiliana na ugonjwa
huo iwapo utakithiri.
Awali dalili za homa hii zilionekana
kama za ugonjwa wa ebola.kuvuja
damu, kutapika na joto kali la
mwili.lakini kwa kuwa ebola ni
ugonjwa mpya, homa ya Lassa nayo
bado ipo, ambayo inaelezwa kuwa
kila mwaka watu 300,000 mpaka
500,000 huathiriwa na homa hii na
watu mpaka 20,000 hupoteza
maisha.
Kila nchi iliyoathiriwa na ebola pia ina
ugonjwa wa homa ya Lassa, ijumaa
juma lililopita Dr.Geraldine O'Hara
kutoka Shirika la Madaktari wasio na
mipaka MSF ameiambia BBC kuwa
mmoja wa wafanyakazi wenzake
alipoteza maisha ingawa walifanya
kila jitihada kuokoa maisha yake.
Inaelezwa kuwa Nigeria huenda
ikakumbwa na mlipuko wa ugonjwa
wa Lassa, wakati huu ikiwa ni
majuma kadhaa baada ya kufanikiwa
kukabili ugonjwa wa ebola.
Kuna tofauti moja kubwa kati ya
ebola na homa ya Lassa.Lassa
husababishwa na Panya ambao
hubeba vijidudu kwenye maeneo ya
makazi ya watu na kwenye hifadhi za
vyakula hasa kipindi cha Kiangazi.
Profesa Robert Garry kutoka Chuo
cha Tulane amefanya utafiti kuhusu
ugonjwa huu kwa amesema
Kumekua na ripoti kadhaa za watu
kuugua homa ya Lassa nchini Sierra
Leone.
Lassa huambukiza lakini si kila
anayeambukizwa huwa katika hali
mbaya, ugonjwa huu hausambai kwa
kasi kama ebola.

No comments:

Post a Comment

.