Monday 10 November 2014

MAMA AMNYONGA MWANAE WA MIAKA MIWILI NA KUMZAMISHA ZIWA VICTORIA.

bby itemsWapo wanawake ambao wamekua wakihangaika usiku na mchana ili waweze kupata watoto lakini wapo wengine ambao wamekua wakipewa watoto hao na Mungu lakini hukufuru kwa kuwaua kwa sababu tu hawana uwezo kifedha wa kuwalea na wengine kutokua tayari kuitwa mama.
Ni kawaida sana kwa sasa kusikia mama kamuua mwanaye aidha kwa kumtupa akiwa hai ama kumuua kabisa ili aweze kupoteza ushahidi na kuendelea na mambo yake.
Huko Sengerema,Mwanza mama mmoja Magreth Martini mwenye miaka20 amenusurika kuuawa na watu wenye hasira kali baada ya kumnyonga mwanaye wa miaka miwili kisha kumzamisha katika Ziwa Victoria.
Mama huyo anatuhumiwa kuchukua uamuzi huo kwa madai ya mwanaye kumnyima muda wa kujirusha kwa kufanya mambo yake binafsi ambapo wanakijiji waliona mwili wa mtoto huyo ukielea kando kando ya Ziwa hilo huku mama yake huyo akiendelea na huduma kwenye mgahawa wa pembezoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlolowa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa baada ya kuhojiwa na Polisi alikiri kumnyonga na kumzamisha mtoto wake Ziwani.
Mtendaji wa kijiji Charles Subira alisema alifanya juhudi za ziada kuokoa maisha ya mtuhumiwa huyo toka kwa wananchi waliokua na hasira kutaka kulipiza kisasi ambapo walitaka kumuua kisha mwili wake kuuchoma moto.

Alisema awali mama wa mtoto huyo alimtelekeza mwanaye kwa jirani na siku moja kabla ya tuko alikwenda na kudai anataka kwenda naye kazini ndipo baadaye mwili wa mtoto huyo ukakutwa unaelea pembezoni mwa Ziwa Victoria.
Mganda Mfawifdhi wa Hospitali ya Buhama Eliud Bahama  alithibitisha kupokea mwili wa mtoto huyo na kusema kifo chake kimetokana na kunyongwa shingoni.
LIKE PAGE NA TUPE MAONI YAKO KUHUSU MAMA HUYU 

No comments:

Post a Comment

.