Saratani ya ubongo mara nyingi hujulikana kama uvimbe katika ubongo ambao husababishwa na kukua kwa kasi na bila mpangilio wa seli hai katika ubongo. Hii inaweza kusababishwa na kusambaa kwa saratani nyingine kutoka katika sehemu za mwili au saratani inayoanzia katika seli za ubongo. Saratani huu husababishwa na mionzi hatari inayotokana na matumizi ya x ray kwa muda mrefu pamoja na mionzi ya simu. Pia inaweza kutokana na kusambaa kwa saratani ya matiti, moyo, ini n.k pamoja na kemikali zinazotokana na matumizi ya plastic kwa muda mrefu au upungufu wa kinga mwilini.
DALILI.
Saratani hii huanza kuwa na dalili kwa kuhathiri ubongo pamoja na kusambaa katika sehemu za karibu na ubongo kama kifafa, kutokuona vizuriau kuona mawenge, maumivu makali ya kichwa au kipanda uso, kutapika, kupoteza fahamu,kuchanganyikiwa, mabadiliko ya tabia na kushindwa kutembea vizuri.
VIPIMO NA TIBA
Saratani hii ugunduliwa kwa kufanyiwa uchunguzi katika mfumo wa fahamu, vipimo vya CT, MRI na uchunguzi wa tishu katika ubongo(Brain biopsy) ambavyo ki ukweli huwa ni gharama sana.
Tiba yake huwa ni upasuaji wa mapema kuondoa uvimbe, mionzi kupunguza uvimbe, pamoja na dawa ambazo huyeyusha na kupunguza uvimbe wakati huwezekano wa kupona hutegemea aina ya saratani, kiasi gani imesambaa, umri na afya ya mgonjwa.
KUISHI MAISHA MAREFU NA UGONJWA HUU.
Tumia dawa za kupunguza uvimbe kama ulivyoelekezwa hosipitali.
Punguza uzito na pata muda mwingi wa kupumzika
Epuka kemikali sumu kama dawa za kushafishia vyoo, vumbi, dawa za kuua wadudu na moshi kutoka viwandani.
Kula lishe bora ambayo huongeza kinga ya mwili.
kufanya mazoezi mepesi mara kwa mara na kuepuka msongo wa mawazo.
BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA WASILIANA NASI KWA MSAADA ZAIDI.
No comments:
Post a Comment