Sunday 16 November 2014

SOMA HII MUHIMU SANA KWA AFYA YAKO.

Kemikali zinazopatikana katika baadhi ya bidhaa ambazo hutumiwa
kila siku kama vile dawa ya kusugua meno, sabuni na mafuta ya
kujikinga kutokana na miale hatari ya jua zinaweza kuharibu mbegu
za uzazi za wanaume.

Kwa mara ya kwanza watafiti wanaonya kuwa bidhaa hizo zina
uwezo wa kuanthiri uwezo wa mbegu za uzazi za wanaume
kuzalisha mwanamke. Wanasayansi hao wanasema kwamba bidhaa hizo zina kemikali
ambazo zinachangia matatizo ya uzazi kwa wanaume katika nchi za
magharibi. Kemikali zinazopatikana katika dawa za kusugua meno zinasemekana
kuharibu nguvu za mbegu za kiume kuweza kuzalisha. Takriban mwanamume mmoja kati ya sita aliyeoa nchini Uingereza
anakumbwa na tatizo la kuzalisha na tatizo la utasa ndio kiini
kikubwa cha hali hiyo. Uchunguzi huu ulifanywa na watafiti kutoka Uingereza na Uholanzi
na walifanyia uchunguzi kemikali 100 kila siku huku wakigundua
kuwa thuluthi moja ya kemikali hizo ziliathiri uwezo wa Manii kufikia
katika mayai ya mwanamke. Dawa ya meno inaweza kuathiri mbegu za uzazi Utafiti huu uliandikwa katika jarida la afya la EMBO na watafiti
wanasema nyingi ya kemikali hizo hatari zinapatikana katika mafuta
yanayotumiwa kujizuia na miale hatari ya jua. Kemikali nyingine inajulikana kama Triclosan, ambayo inapatikana
katika sabuni na dawa ya kusugua meno. Uchunguzi wa maabara ulionyesha kuwa kemikali hizo zinaathiri
uwezo wa Manii ikitafuta mayai ya mwanamke kuweza kuizalisha. Kadhalika kemikali hizo pia zinaharibu kabisa manii kiasi cha kukosa
hisia kwa homoni za mwanamke. Mabadiliko haya yanapotokea kwa mbegu za kiume, huifanya kuwa
vigumu kuweza kuzalisha. Watafiti hao wanasema kuwa mchanganyiko wa kemikali hizo ni
hatari zaidi kwa mbegu hizo. Kemikali hizi hujulikana kama kemikali zinazoathiri jinsia kwa sababu ni
sehemu ya kemikali zinzzoathiri homoni za mwili wa mwanamume. Mwaka jana shirika la afya duniani lilihusisha kemikali hizo na saratani
ya matiti na pumu.

SOURCE JF Doctor
BOFYA HAPA KUWASHIRIKISHA MARAFIKI 

No comments:

Post a Comment

.