Thursday, 6 November 2014

KWA WANAWAKE WANAOTOKWA NA DAMU KIPINDI CHA UJAUZITO.

Kutokwa na damu wakati wa ujauzito katika zile wiki 12 za awali za ujauzito siyo kitu cha ajabu, kwani 20 % hadi 30 % ya wajawazito hupata/huona dalili hiyo. Lakini kwa kuwa ziko sababu nyingi za kutokwa na damu wakati wa ujauzito, unashauriwa uende kituo cha huduma za afya kufanyiwa uchunguzi, kupata muda mrefu wa kupumzika, kuepuka kazi nzito na kupata ushauri wa uhakika.


Kutokwa na damu wakati wa ujauzito baada ya wiki 13 hadi ya 24, na wiki ya 25 hadi ya 36 ni dalili mbaya na mjamzito anashauriwa kuenda haraka sana kwenye kituo cha huduma za afya kufanyiwa uchunguzi na kupata ushauri wa uhakika. Kutokwa na damu wakati wa ujauzito wakati huu yaweza kuwa ni dalili ya ectopic pregancy, mlalo mbaya wa placenta (placenta previa), miscarriage, uvimbe nk

No comments:

Post a Comment

.