Monday 3 November 2014

KIJANA ALIYESHINDWA KULA KWA MWAKA MMOJA.

Landon Jones mwenye umri wa
miaka 12 ni kijana aliyepoteza
hamu ya kula pamoja na ile ya
kunywa kwa mwaka mmoja kufikia
sasa nchini Uingereza.
Mnamo mwezi Octoba mwaka
uliopita kijana huyo aliamka akiwa
hana hamu ya kula wala kunywa.
Landon ambaye alikuwa kijana
mwenye nguvu aliyependa
kukimbia,kupeleka baisklei pamoja
na kucheza na marafiki zake.
Madaktari katika hospitali tano tofauti
wameshindwa kubaini ni nini
kinachomsumbua kijana huyo.
Wazazi wake Michael na Debbie
wametafuta tiba kwa udi na uvumba
lakini majaribio yote ya matibabu
yameshindwa kufaulu.
Wataalam wanaamini kwamba
Landon ni kijana aliye na ugonjwa wa
kipekee ulimwenguni.
Katika kipindi cha mwaka mmoja
kijana huyo amepoteza kilo nyingi za
mwili wake .
Wazazi wake wamejaribu kila
wawezalo kumshawishi mwana wao
kula ,lakini ni nadra kwa kijana huyo
wa miaka 12 kutia chochote
mdomoni.
Vile vile katika kipindi cha mwaka
mmoja amekosa masomo kwa
takriban siku 65 mbali na kuwa
wazazi wake wanasema kwamba
hajakimbia kwa miezi kadhaa
sasa,huku akilazimika kuwaangalia
rafikize kutoka dirisha la nyumbani.
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

.