Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa masuala ya afya na
lishe nchini Marekani umebaini kuwa “kifungua
kinywa huupa moyo afya na kuuepusha na magonjwa ya mshtuko wa moyo.”
Utafiti wao uliowahusisha wanaume 27,000 wenye umri kati ya
miaka 45-82 ulionyesha kuwa wale wasiokula kiamsha kinywa wako katika hatari ya
matatizo ya moyo. Wakati wa utafiti huo, zaidi ya watu 1,500 waliathirika
kutokana na mshtuko wa moyo.
Utafiti huo ulithibitisha kuwa watu waliokosa kifungua
kinywa wako katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya moyo kwa asilimia 27
kuliko wale wanaokula asubuhi.
Ukizingatia utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Harvad
kitivo cha afya ya jamii kilisema kuwa: “kukosa
kiamsha kinywa kunasababisha mwili kutumia nguvu nyingi zaidi kuliko kawaida.”
Sambamba na utafiti huo, taasisi ya matibabu ya moyo nchini Uingereza imebaini
kuwa “kiamsha kinywa huwazuia watu kula
vitu vyenye sukari kabla ya chakula cha
mchana.”(http://www.bbc.co.uk/swahili/kwa_kina/2013/07/130723_kiamsha_kinywa.shtml).
Kupata kifungua kinywa kwa mtu wa kipato cha chini
inawezekana...si lazima iwe kama picha inavyoonyesha, ni muhimu kuzingatia
makundi ya vyakula unayotakiwa kula kulingana na kipato chako.Yote tisa,
kifungua kinywa ni muhimu sana kwa afya yako.
No comments:
Post a Comment