Friday 7 November 2014

MAZOEZI MUHIMU KWA AKINA DADA NA MAMA.





 
Wanawake wa zamani walikuwa wakifanya shughuli nyingi sana kama kutembea kwa muda mrefu ili kufika sehemu wanazotaka jambo ambalo lililkuwa likiwasaidia kujifungua salama. 

Ila wanawake wa siku hizi mara nyingi tunafanya kazi ofisini, tunaenda kwa magari, unafika ofisini umekaa kwenye kiti, umerudi nyumbani unakaa tena kwenye kochi ukila chakula umekaa kwenye meza ya chakula kwenye kiti, kazi nyingi zimerahisishwa na mashine na hata wasaidizi wa nyumba unaishia kulala tu au kukaa tena kwenye kochi mbele ya tv, computer au simu.
wanawake mnashauriwa kutenga muda maalum wa kufanya mazoezi ili kufidia kuupa mwili mazoezi ya kutosha. Na ni muhimu sana kwa mwanamke mjamzito kufanya mazoezi maalum ili kusaidia kupanua na kuongeza njia ya uzazi. Na sio kufanya mazoezi yoyote yale bali yale muhimu ambayo yatasaidia kuongeza na kupanua njia na misuli maalumu ya uzazi kama yafuatayo.

No comments:

Post a Comment

.