Vinavyohitajika:
1.Avocado moja lililoiva vyema.
2.Mtindi kijiko kimoja cha chakula.
3.Asali asilia (natural honey).
4.Maji ya ndimu/limao.
Namna ya kutayarisha:
Kata Avocado katika vipande viwili, ondoa kokwa na menya.
Changanya
avocado ulomenya na mtindi, asali na maji ya ndimu au limao. Koroga
mapaka upate mchanganyiko wa hali moja halafu weka pembeni.
Chukua
maganda ya avocado na kwa upande wa ndani ya maganda hayo sugulia uso
na shingo. Kufanya hivyo husaidia kuondoa seli zilizokufa na ngozi
zilizoharibika. Pia huutayarisha uso kwa ajili ya mask.
Kisha paka mchanganyiko uliotayarisha usoni na shingoni (sio machoni).
Subiri kwa dakika 15 na kisha osha kwa maji vuguvugu.
Usitumie mask ya Avocardo kama ngozi yako ni
yenye mafuta na kutoka chunusi. Kwani Avocado kwa kuwa na mafuta mafuta,
maska ya tunda hilo hufaa zaidi kwa wenye ngozi kavu na za kawaida. Kwa
ajili ya ngozi zenye mafuta unaweza kutumia mask zinazotengenezwa kwa
udongo, ndizi,tango, chai na kadhalika.
BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA WAELIMISHE MARAFIKI
No comments:
Post a Comment