Wataalamu wa macho wanashauri kuwa matumizi kupindukia ya mara kwa mara
ya simu za kisasa (Screen touch Smartphone), TV pamoja na Computer yana
madhara sana kwa afya ya macho kutokana na kuwa na mionzi ya Blue violet
ambayo huweza kusababisha upofu wa macho.
Pia matumizi ya muda mrefu ambayo husababisha kuharibu au kukosa
usingizi husababisha athari za kisaikologia kama mawazo, hasira na wasi
wasi unapokuwa mbali na simu yako.
Pia matumizi ya muda mrefu wa simu za kisasa husababisha maumivu ya
kichwa, shingo, na mabega kutokana na kupunguza mzunguko wa damu katika
sehemu hizi.
Hata hivo tunashauriwa kufanya uchunguzi wa macho mara kwa mara ili
kugundua matatizo haya kabla hayajafikia katika hatua ya upofu ambayo
huwa ngumu na ghalama kutibika.
No comments:
Post a Comment