Picha ya mtu mwenye mafua. |
Mafua ni ugonjwa
unao sumbua watu
kila mwaka, hasa yanayo
anza kutokea mabadiliko
ya hali ya
hewa kutoka msimu wa
kiangazi kuingia masika.
Orodha ya vyakula
vifuatavyo vimeelezwa kuwa
na uwezo mkubwa
wa kuimarisha kinga
ya mwili na kupambana
na maambukizi mengine
kwa kuwa na
kiasi kikubwa cha
protini na virutubisho
vingine.
SUPU YA KUKU
Supu ya kuku wa
kienyeji inaelezwa kuwa
na virutubisho vinavyo
saidia kupunguza utokaji
wa makamasi.
Supu ya kuku |
Utapata virutubisho
vingi zaidi ukitengeneza
supu ya kuku
kwa kuchanganya na
mboga za majani. Weka
chumvi kiasi kidogo
katika supu hiyo.
VITUNGUU SAUMU
Vitunguu saumu vina
kirutubisho aina ya ‘
allicin’ ambacho kina
uwezo wa kutoa
kinga dhidi ya
magojwa mbalimbali ya
kuambukiza.
Vitunguu Saumu |
Kitunguu saumu kinatoa
kinga halikadhalika kinapunguza
muda wa mtu
kuumwa na mafua.
Tumia kitunguu hicho
kwa kupika kwenye
chakula au kwa
kutafuna punje.
CHAI
Chai hasa ya
kijani, ( Green Tea ) ina virutubisho
vya kuimarisha kinga
ya mwili .
Chai Ya Kijani |
Utafiti wa hivi
karibuni ulio fanywa
na jarida moja
la masuala ya
virutubisho nchini Marekani ( Journal Of the
American College of Nutrition )
umeonyesha kuwa watu
wanao tumia chai
kwa mpangilio maalumu, hawasumbuliwi mara
kwa mara na
mafua pamoja na
magonjwa mengine ya
kuambukiza, huwa salama na mafua au
siku za kuumwa mafua
hupungua kwa asilimia
36 ukilinganisha na wale wasio
kuwa na kinga
imara.
Hata hivyo,
tahadhari inatolewa kwa watoto wa
shule kutokupewa kiasi kingi
cha chai kwa siku.
Unywaji wa kikombe
kimoja kwa siku
kwa motto wa
shule siyo mbaya.
Kwa mtu mzima,
usizidishe vikombe vitatu kwa
siku.
Ikumbukwe kuwa,
chai inapotumika kwa
wingi kupita kiasi, huweza
kusababisha pia tatizo
la kukosa choo
kwa muda mrefu.
Kunywa kiasi kwa
afya yako.
MACHUNGWA, PILIPILI
KALI
Utafiti
unaonyesha kwamba, ulaji wa
vyakula vyenye Vitamin
C kwa wingi kila
siku husaidia kuondoa
au kuzuia ugonjwa
wa mafua.
Machungwa |
Miongoni mwa vyakula
vyenye kiwango kikubwa
cha Vitamin C ni
pamoja na machungwa, mboga za
majani aina ya
Brokoli na pilipili kali.
Pilipili Kali |
Ili kupata kiasi kingi
cha Vitamin C, inashauriwa machungwa
yaliwe pamoja na
nyama zake za
ndani au kunywa
juisi yake.
ASALI
Kama inavyo julikana, asali ni
tiba ya matatizo
mengi ya kiafya, miongoni mwa
hayo ni pamoja
na mafua.
Asali inasaidia kuondoa
kikohozi na muwasho
kwenye koo. Halikadhalika, asali inaweza
kutumiwa na watoto wadogo
kama dawa.
Watoto wanao ruhusiwa kutumia asali
kama tiba ni wa umri
wa kati ya
miaka 2 hadi
5.
Hawa dozi yao
ni nusu kijiko
kidogo cha asali, wenye umri wa
miaka 6 hadi 11
wapewe kijiko kimoja
kidogo na wenye
umri wa kuanzia
miaka 12 hadi
18, wapewe vijiko vidogo
viwili vya asali
wakati wa kulala.
MTINDI
Kutokana na kiwango kikubwa cha
protini ilicho nacho, Mtindi ni
chakula kingine kinachofaa
kuliwa na mtu
mwenye mafua ili
kupunguza siku za
kusumbuliwa na ugonjwa
wa kukohoa.
Wataalamu
wanakubaliana kuwa, ulaji wa ‘chocolate’
nyeusi ( Dark Chocolate ), huimarisha kinga
ya mwili, hivyo inapoliwa
na mgonjwa wa
mafua, huweza kumpa ahueni
mgonjwa kwa namna
moja ama nyingine, na
pia huwa kinga
kwa magonjwa mengine.
PWEZA
Samaki aina ya
pweza wana virutubisho vingi
vya kuongeza kinga ya
mwili yenye uwezo
wa kupambana na
bacteria pamoja na
virusi vya mafua.
Kiasi kidogo cha
pweza, awe wa kukaangwa
au kuchemshwa kama
supu, anafaa kuliwa
mara kwa mara
kukmarisha kinga ya
mwili.
VIAZI VITAMU
Kirutubisho
hicho huwa ni
muhimu kwa ustawi
na uimarishaji wa
kinga mwilini na
kinapatikana kwa wingi kwenye
viazi vitamu na vyakula
vingine kama vile
karoti, maboga na mayai ( kiini)
Kwa ujumla ,
suala la
kuimarisha kinga ya
mwili ni muhimu
kwa afya zetu.
No comments:
Post a Comment